Producer mkongwe na C.E.O wa MJ Records Master J amesema kuwa wasanii wa Tanzania wanawaibia watayarishaji wa muziki.
Master
J amefunguka kwenye ‘The Jump Off’ ya 100.5 Times Fm wakati akijadili
na Jabir Saleh aka Kuvichaka na Dvj D_Ommy kuhusu haki za wasanii na
watayarishaji wa muziki hapa nchini.
“Huwezi
kuchukua wazo langu uende kulitumia kutengeneza hela halafu uniambie
kwamba ‘bwana mimi sikupi kitu’, wasanii ni wezi tu Bongo.” Amesema
Master J.
Unaweza
kudhani labda aliteleza kidogo kusema hilo, lakini kwa kuwa ana uhakika
na anachokisema, producer huyo mwenye mchango mkubwa kwa muziki wa
kizazi kipya hapa nchini aliweka mkazo kwenye maneno yake.
“Watu
wanaogopa kuongea, mimi ngoja niongee tu ukweli, wasanii wa Bongo ni
wezi. Kitu wanachokifanya ni wizi. Unajua mwizi anakaaga kimya, lakini
wanakwenda kwenye media wanaropoka ‘nimeingiza million 300 (kwa
kutumikia haki ya Lamar bure na simpi kitu)’. Yaani unaiba halafu
unaenda unatangaza kwenye media!” alifunguka Master J.
“Hata
hawaogopi! Walivyokuwa hawajui kwamba sheria hairuhusu kufanya hivyo,
na kiukweli akiamua kupania anapata cha kwake, sema tu maproducer
hawafuatilii. Lakini wanavunja sheria kabisa na ni wezi. Huwezi kufanya
hivyo halafu unaenda unatangaza, kaa kimya...kula na kipofu. Sio sawa
wanavyofanya.” Aliongeza kwa msisitizo.
No comments:
Post a Comment