![]() |
Man Kichefu |
Kupitia ukurasa wa Facebook msanii wa hip hop wa mkoani
Iringa Man Kichefu, leo ameandika, ‘jana nliitwa na eddo ebony.fm cha
kushangaza alinivamia na kuanza kunipiga akidai nimemchafua! Poa mi sina noma
ila nachoweza kusema its only the weak need to prove his strength through
force! My mom hits more than anyone I ever met!”
Kufuatia status hiyo tumempigia simu Man Kichefu ili
atueleze sababu ya yeye kupigwa na mtangazaji huyo.
“Kuna harakati fulani za muzki wa nyumbani hapa, unajue
eeh, jamaa (Ebony Fm) wanatudiss sisi wasanii wa hapa. Kwahiyo kitu kilichokuja
kufanyika kuna ngoma fulani sababu sisi kuna studio yetu tumefungua ,
tumejichanga tu mimi na mshikaji wangu tumefungua studio ,tumetengeza ngoma
moja kwahiyo hiyo ngoma tuliyoitengeza inaitwa ‘Himaya ya Mkwawa’ inaelezea
historia ya muziki wa Iringa na watu wa Iringa wale wanausuport muziki na wasio
usupport. Baada ya ngoma hiyo niliiyoifanya sababu nimeiweka tu kwenye internet
jamaa wakaichukua ile ngoma kitu kama wakaisikiliza hivi lakini mimi nikawa sijui.
Nikawa napewa tu taarifa kuwa jamaa anakutafuta kaongea
sana redioni. Mwisho wa siku juzi akanipigia simu mimi nikaipokea tu kwa roho
safi, ‘vipi bro, fresh fresh’ akaniambia
ebana na shida na wewe njoo ofisini.
Nikamwambia poa mimi nikaenda tu kwa roho safi. Ndio hivyo
yanii nimeenda ofisini jamaa akaniita akaanza kunitukana pale anadai nimemchafua,
kanivamia akaanza kunipiga.
Na baadhi ya wafanyakazi wengine yaani walikuja wakawa
wananishika wananiambai ebana twende huku tukaongee. Pale ofisini kwao kuna
sehemu moja nyuma ya ofisi kuna kibanda cha kupumzikia hivi, akaniita pale njoo
tuongee.
Nimefika hapo ndo akaanza kunishambulia sasa mimi nikaona hili eneo si
zuri sababu ni nyuma ya ofisi, nikakimbia nikaja nyuma ya ofisi.
Nimekuja mbele ya ofisi baadhi ya wafanyakazi wenzake
wakaja wakanishika bana twende huku wakawa wananirudisha tena kule ambako jamaa
alikuwa ananipiga yaani!
![]() |
Eddo mtangazaji wa Ebony Fm |
Kitu nilichokifanya mimi, nimefungua kesi polisi
kwasababu ya ulinzi wangu wa mbele au kitu chochote kitakachoenda kule mbele
lakini pia mimi sitaki nimfunge ama nimfanye lolote yaani.”
Tumemtafuta Eddo ili aeleze kwa upande wake lakini simu
yake haipatikani.
No comments:
Post a Comment