Video mpya ya Diamond 'KESHO' ambayo imeanza kuonekana kwenye mtandao wa internet jana usiku, ilivuja kimakosa na kusambaa kwa watu.
Diamond kupitia kipindi
cha Power Jams cha East Africa Radio leo amesema kampuni ya Ogopa Djs ya
nchini Kenya ambao ndio wametengeneza video hiyo
walii-upload video hiyo youtube kama njia ya kumtumia Diamond na uongozi wake waitazame kwanza kama iko sawa kabla ya makabidhiano rasmi.
Akaendelea kumpa mkasa huo deejay jona kwamba baada
ya yeye Diamond kutumiwa link ya video hiyo na kuitazama aligundua baadhi ya
makosa na kuwaomba Ogopa warekebishe, na baadhi ya makosa ni pamoja na
titles za video zinazoonyesha producer wa wimbo ni Wasafi Entertainment
na huku aliefanya wimbo huo ni Marco Chali wa Mj Records.
Diamond aliendelea
kufunguka kuwa baada ya kukubaliana na Ogopa waliiondoa kwenye youtube
video hiyo lakini ilikuwa too late kwani tayari watu walikuwa wameishai
download na kuiweka katika akaunti zao binafsi.
Diamond alimalizia kwa
kusema video rasmi ya 'Kesho' itatoka rasmi Ijumaa ya wiki hii na pia
bado yeye na management yake wanajadiliana kama itoke video na audio
pamoja ama video peke yake.
No comments:
Post a Comment