Baby's mama wa Jay-Z, the queen herself Beyonce Knowlence
amepata deal ya kulipamba jarida la GQ kwa picha kadhaa zinazoonesha mwili wake
wenye mvuto licha ya kuwa hivi sasa ni mama wa mtoto mmoja.
Beyonce ameliambia jarida hilo kuwa anafurahia sana kuona
kuwa ameweza kuzifikia ndoto zake za kuwa alama ya mafanikio na uwezeshwaji wa
wanawake duniani, lakini anapata ugumu wa kujua ni kiasi gani ameweza
kuwa-influence wanawake hao.
![]() |
Muangalie Queen Beyonce na pozi matata, bado anakimbiza sana tu: |
Mama Blue Ivy alifunguka zaidi, "Wakati naandika nyimbo
za Destiny's child, kilikuwa kitu kikubwa sana kwangu kuwa mdogo vile na kuweza
kucontrol. Na lebel yetu kwa wakati ule haikujua kama tungekuja kuwa na
mafanikio kiasi kile, kwa hiyo walitupatia nafasi ya kujicontrol. Na nikaiweza.
Ni lengo langu katika maisha yangu kuwa mfano wa namna hii.
No comments:
Post a Comment