
Taarifa kutoka vyombo kadhaa vya habari ambazo pia zimesibitishwa rasmi na msanii mwingine mkongwe katika tasnia hiyo Suzane Lewis 'Natasha' zinasema kuwa ‘Sajuki’ amefariki dunia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alikokuwa kufuatia tukio la kudodoka jukwaani jijini Arusha mwishoni mwa mwaka uliopita, wakati alipokuwa akitoa salamu za shukurani kwa Watanzania kumuombea na kumchangia kwa hali na mali wakati alipokuwa kwenye matibabu nchini India.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen
No comments:
Post a Comment