 |
HAPA NI IRENE UWOYA NA KWA
NYUMA NI KING MAJUTO WAKIFATILIA HIZO TUZO KWA UMAKINI
KABISA |
WAIGIZAJI nguli katika tasnia ya filamu hapa
Tanzania, Ray, JB, King Majuto pamoja na Irene Uwoya wamefunika mbaya katika
tamasha la utoaji tuzo huko nchi Rwanda ambapo msanii kama Irene Uwoya ilibidi
jina lake la asili lipotee na kujikuta akikumbushwa enzi za nyuma alivyotesa
katika filamu iliyotamba na kuwa gumzo ya Oprah on Sunday.
Matangazo
katika redio televisheni jina lilokuwa likisikika ni Oprah umugore wa Katawuti
wakimananisha kuwa Irene mke wa mchezaji wa mpira Ndikumana, jina la Oprah
limekuwa ni jina maarufu nchini Rwanda kufuatia filamu ya Oprah on Sunday
iliyowashirikisha wasanii nyota marehemu Steven Kanumba na Vincent Kigosi
‘Ray’.
Wanyarwanda walilipuka ukumbi huku wakiita Oprah na Ray wakimwita
Kigozi badala ya Kigosi, tuzo hizo zilizopewa jina la Rwanda Movie Awards
zikilenga kuwatunuku wasanii wa filamu wa nchi hiyo na wasanii kutoka Bongo
wakiwa kama watu mashuhuri waliofika kutoa zawadi kwa washindi walichaguliwa
Rwanda Movie Awards.
 |
JB
NA RAY WAKIPEANA MAWILI MATATU |
 |
RAY |
 |
RAY, IRENE & KING MAJUTO
|
No comments:
Post a Comment