Friday, September 12, 2014

Hii ni kwa akina dada Je? unakipaji cha Mitindo au Uigizaji? ingia hapa kupata mchongo

Wewe  ni msichana  mwenye  kipaji  cha  mitindo  lakini  haujui  uanzie  wapi? Wewe  ni  msichana  mwenye  kipaji  cha  kuigiza ? Unatafuta  nafasi  ya  kuigiza   kwenye  filamu ? Kama  jibu  ni  ndio  basi  hii  ni  habari  njema  sana  kwako.
Kampuni  inayo  jihusisha  na  ku- manage   wanamitindo  pamoja  na  wasanii  wenye  vipaji  mbalimbali  inatangaza  nafasi  za kazi  zifuatazo:
A.     WANAMITINDO  WANAWAKE  ( FEMALE  MODELS )
Sifa  za  wanamitindo  wanao  hitajika :
i.Awe  na  elimu  ya  kuanzia  kidato  cha  nne  na  kuendelea.
ii.Awe  wa  jinsia  ya  kike
iii.Awe  anaweza  kuwasiliana  kwa  ufasaha  kwa  lugha  za  Kiswahili  na  kiingereza.
iv. Awe   na  passion  na  kazi  ya  mitindo.
MAJUKUMU    YA     KAZI   :
Kufanya  kazi  za  mitindo   katika projects  mbalimbali  za  kampuni  zilizopo  ndani  na  nje  ya  mkoa  wa  Dar  Es  salaam  pamoja  na  nchi  jirani.
B. WASANII   WA   FILAMU.
Sifa  za  wasanii  wanao  hitajika :
i.Awe  wa  jinsia  ya  kike.
ii.Awe  na  kipaji  cha  ukweli  cha  uigizaji.
iii.Elimu  ya  kuanzia  kidato  cha  nne  na  kuendelea.
MAJUKUMU  :
Kushiriki  katika  filamu  mbalimbali  zinazo  tolewa  na  kampuni  mbalimbali  za  utayarishaji  filamu.
JINSI   YA  KUTUMA  MAOMBI   YAKO
1.  Andika  maombi  yako kupitia  barua  pepe  yetu  ambayo  ni  : neemarecruitmentagency@gmail.com
Maombi  yako  yaelekezwe  kwa  Mkurugenzi Mtendaji, Neema  Recruitment  Agency.
2.   Leta  maombi  yako  moja  kwa  moja  katika  ofisi  zetu  zilizopo  katika  eneo  la  CHANGANYIKENI  karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU  mbele  ya  CHUO  KIKUU  CHA  DAR  ES  SALAAM.
JINSI   YA  KUFIKA  OFISINI  KWETU :
Kufika  ofisini  kwetu  panda  daladala  za  UBUNGO-CHANGANYIKENI  kisha  shuka  kituo  kinaitwa  TAKWIMU  ukifika  hapo  tembea  hatua  ishirini  mbele  kisha  tazama  upande  wako  wa  kulia  utaona  ofisi  imeandikwa  RAEFO  TANZANIA.

Kwa  maelezo zaidi  piga  simu 0784406508.

No comments: