
Ni miongoni mwa Maproducer wanaofanya vizuri katika tasnia ya muziki wa Tanzania anaitwa Emmanuel Mkono a.k.a Nahreel ambaye alianza harakati zake katika studio za Kama Kawa chini ya G solo ambapo alipata fursa ya kukutana na wasanii wengi kama Roma, KalaJeremiah na wengine wengi.
Nahreel ametengeneza nyimbo nyingi ambazo zimefanya vizuri katika vituo mbalimbali vya radio na Televisheni, hizi hits 10 ambazo amezitengeneza katika studio
tofauti.
1.Niaje ni vipi – Joh Makini & Nikki wa Pili
2.Tanzania – Roma
3.Riz One – Izzo Bizness ft Mwasiti
4.Kiujamaa – Nikki wa Pili ft Pipi
5.Stimu zimelipiwa – Joh Makini
6.Nje ya Box -Nikki wa Pili ft G Nako na Joh Makini
7.Love Me -Izzo Bizness ft Barnaba na Shaa
8.Gere – Weusi
9.Usinibwage- Navy Kenzo
10.Chelewa – Navy Kenzo
Hizo ndio ngoma 10 kali amabazo Nahreel anazikubali lakini zipo na nyingine nyingi tu zaidi.
Pia Nahreel kwa sasa anampango wa kufungua studio yake ambapo ni kwa muda mrefu amelifikiria suala, pia katika upande wa jina la studio hatocheza mbali na jina lake yaani Nahreel, kwa iyo studio huenda ikaja kuitwa Nahreel Music na kwa upande wa eneo la kuiweka studio hiyo zipo sehemu nyingi ila bado hajachagua rasmi aiweke wapi
Pia studio hiyo itakuwa inachukua record lebel kwa wasanii hasa wasanii wachanga ambao wanachipukia ili aweze kuwaandaa na kukaa nao kuwasoma nini wanacho kipya ili waweze kufanya vizuri kama ilivyo kwa wasanii wakubwa wenye majina.
Mbali na hayo kama ulikuwa hujui sammisago.com ikuarifu kwamba Nahreel ni mshabiki mkubwa wa Barcelona huku mpenzi wake Aika yeye akiwa ni shabiki wa Arsenal, kazi ipo hapo.
No comments:
Post a Comment