Tuesday, February 24, 2015

Iringa yamiminwa mabomu ya machozi eneo la Ilula wilayani kilolo

Polisi imetumia mabomu ya machozi leo katika eneo la Ilula Wlayani Kilolo Mkoani Iringa wakati ilipojaribu kutuliza jazba za wananchi waliokuwa wakiandamana kulaani kile kilichodaiwa kufariki dunia kwa mfanyabiashara mmoja kwenye eneo hilo.

wananchi hao walichukua udhibiti wa barabara kuu ya Iringa Morogoro kwa kuchoma matairi katikati ya barabara hali iliyotatiza shughuli za usafiri kwenye barabara hiyo.
Kulingana na taarifa kutoka eneo la tukio rapsha hizo zimejiri baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa mfanyabishara Mmoja ameshambuliwa hadi kufa na polisi.
Hata hivyo hapajawa na duru huru za taarifa kuthibitisha tukio hilo.
Katika tukio hilo inadaiwa kuwa askari mmoja amejeruhiwa.
Una maoni gani?

No comments: