Nimerudi Shule Ndio Maana Nipo Kimya' Asema HAFSA KAZINJA >>>>>>>
Msanii wa Zouk nchini Tanzania Hafsa
Kazinja aliyewahi kutamba sana na wimbo
wake wa 'PRESSURE'aliyoshirikiana na BANANA ZORRO aliongea na Millard Ayo katika kipindi cha
Amplifaya na kumueleza sababu zilizopelekea
kuwa kimya kwenye tasnia ya muziki wa Bongo
Fleva. “Of course nipo kimya kwenye maradio ila
matamasha nafanya kama kawaida naweza
nikawa kimya kwenye media lakini
kazi zangu
bado zinatambulika nje na ndani ya nchi kwa
hiyo bado nafanya, lakini kitu ambacho naweza
sema kwanini niko busy sasa hivi niliamua
kurudi shule kwahiyo nilirudi shule mwaka jana
kwa hiyo inataka moyo sana kuanza form one,
form two ni (QT) kwa hiyo mwaka jana Mungu
akanijalia nikafaulu masomo yangu ya form 1
b& 2 sasa hivi niko form 4 nasubiri nimalize
maana mtihani wa form 4 sio mchezo.” “Kwa
hiyo pamoja huku nasoma pia nina wimbo wangu
mpya siwezi kuuzungumzia ila bado upo katika
matayarisho yaani studio,” aliongezea.
No comments:
Post a Comment