Lady Jaydee amekuwa
akiulizwa maswali mengi na fans wake kupitia page zake za social
networks kama facebook na twitter wakitaka kujua mambo mbali mbali ya
kumhusu yeye. Kupitia fan page yake ya facebook ambayo imefanikiwa
kufikisha likes zaidi ya 20,000 mpaka sasa, aliwaahidi kuwa wiki hii
atatoa majibu ya ujumla kwasababu inakuwa ngumu kumjibu mtu mmoja mmoja
sababu ya wingi wa maswali.
Kama alivyoahidi yafuatayo ndio maswali na majibu yake kutoka kwa Lady Jaydee hivyo kama ulimuuliza swali lolote soma hapa chini utakutana na majibu. Hivi ndivyo alivyoandika kupitia blog yake.
Kama alivyoahidi yafuatayo ndio maswali na majibu yake kutoka kwa Lady Jaydee hivyo kama ulimuuliza swali lolote soma hapa chini utakutana na majibu. Hivi ndivyo alivyoandika kupitia blog yake.
"Kama nilivyoahidi kujibu maswali ya walio andika facebook
inbox. Ambayo mengi yao yana fanana, ila kwa yale ambayo yatakuwa hayajajibiwa
ni kutokana na kuwa sikupata majibu yake. Au sina majibu yake kabisa.
1. WANAOOMBA KUFANYA NYIMBO ZA KUSHIRIKIANA, COLLABO/FEAT
Jibu: Ningependa kufanya nyimbo nyingi kwa kushirikiana na
wasanii tofauti, lakini kutokana na ukweli halisi ni kwamba Duniani popote.
Haiwezekani kwa msanii yoyote kufanya Collabo na kila msanii anaeomba kufanya
nae.
Hii ni kutokana na kwamba hata wasikilizaji watachoka
kusikia kila siku sauti ya mtu huyo huyo mmoja
kwenye kila wimbo. Pia wakati mwingine inahitajika kuupa muda katikati
ya Collabo na Collabo
Na ni vema kuwa niwe nimeshawahi hata kumsikia mtu ambae
anaomba nifanye nae wimbo.
Mengi mengine yanakuwa nje ya uwezo wangu.
2. WANAOTAKA KUWA MEMBER WA LA FAMILLE
Jibu: Vigezo vya kuwa member ni kwa wale ambao tumekuwa
tukishirikiana nao kwa mambo mbali mbali katika mitandao, tukazoeana baadae
tukakutana uso kwa uso na kujenga undungu.
Kwasasa tunaiboresha Familia iliopo, watu wazoeane na
kufahamiana kwa ukaribu kabla ya kuongeza members wengine wapya.
Nilifikiria kuunda kundi la pili, litakaloitwa LA FAMILLE 2
Ili lile la kwanza libakie kuwa vile vile, kwakuwa
wamekwisha zoeana sana
Na la pili waunde mazoea pia uwe ni umoja mwingine.
3. WANAOOMBA KUWA NDUGU ZANGU WA HIARI -DADA, KAKA, WADOGO
Jibu: Mtu yoyote ambae anapenda kuwa ndugu yangu kwa hiari
yake anakaribishwa. Tatizo linakuja pale anapotaka tuwe tuna chat muda wote
Ku chat haitawezekana kutokana na muda kuwa hautoshi.
Ila kunipenda na kuniandikia ni vizuri, nikipata muda
nitakuwa najibu, Mkitaka kunitembelea, karibuni Nyumbani Lounge....Sina
maneno....Karibuni sana
4. NAFASI ZA KAZI
Jibu: Kuhusiana na wanaohitaji nafasi za kazi
Mnaweza kuandika e-mail: nyumbanilounge@gmail.com
Huko mtapata majibu kutoka kwa wahusika.
5. MISAADA
Jibu: Kwa wale wanaoniomba misaada ya pesa, za ada, chakula
na mahitaji mengine.
Ukweli ni kwamba uwezo wangu sio mkubwa sana wa kuweza
kumsaidia kila mtu. Japo ningependa kusaidia, na huwa nasaidia pale ninapoweza.
Bahati mbaya maombi yamekuwa mengi kuliko uwezo wangu.
Misaada ya kimuziki naweza kutoa ushauri, ila sina uwezo wa
kumlipia Studio kila msanii mchanga anaeniomba.
Ila mnaweza kwenda kwa wenye Studio zao wakawasaidia
kuwarekodi bure, endapo watavutiwa na kazi zenu ila hiyo itakuwa ni kazi kwenu
kuwashawishi kuwa mna vipaji na mnastahili kusaidiwa bure bila malipo yoyote
6. CD ZINAPOPATIKANA
Jibu: Dar es salaam zinapatikana SHEAR ILLUSIONS - Mlimani City na
NYUMBANI
LOUNGE
Au kwa
walioko mbali piga simu +255 767 884 007/
+255 784 884
007
7. VIDEO MPYA
Jibu: Itatoka baada ya wiki moja
8. PROJECT NYINGINE ZINAZOKUJA
Jibu: Kwa sasa kuna project iko njiani na itaanza kuonekana
mnamo mwezi wa October katikati
Nitawafahamisha pindi kila kitu kitakapokuwa tayari
9. BEI NA BOOKINGS ZA LADY JAYDEE & MACHOZI BAND
Jibu: Wasiliana na Gardner G Habash
+255 767 884
007/ +255 784 884 007
E-mail:
nyumbanilounge@gmail.com
Au fika
Nyumbani Lounge kwa maonano ya uso kwa uso
Asanteni kwa kuniandikia, natumaini nimejitahidi kujibu kama
mlivyotarajia. Nasikitika kwa ubinaadamu wangu pengine kuna maswali sikuweza
kuyajibu, ila uwezo wangu wa kujibu umefikia hapo kwa leo
Kwa mazungumzo ya hapa na pale, na news zozote kunihusu.
Unaweza ku like page yangu www.facebook.com/ladyjaydee
Au nifuate twitter.com kwa jina la JideJayDee
Au niandikie e-mail: judyjaydee@yahoo.com kuhusiana na
maswala ya kimuziki tu lakini sio bookings, wala mambo binafsi.


No comments:
Post a Comment