Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Khaleed Mohamed 'TID' yupo
mahabusu katika Kituo cha Polisi Oysterbay tangu jana usiku baada ya
kukamatwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi msichana
anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake, Mariam Nnauye.
Huyu Ndio Mariam Nnauye. Taarifa zinasema kuwa ugomvi ulianza maisha
club jana usiku baada ya TID kumkuta Mpenzi wake akiongea na mwanaume
mwingine bila ruhusa ya Top In Dar na ndio Top akamvuta mpenzi wake na
kumpiga makofi.Bila kujali mapenzi yao binti huyo alikwenda moja kwa
moja kituo cha polici Osterbay na kutoa taarifa ya kupigwa na Tid.
Baada ya mdada huyo kutoa taarifa kituo cha Polisi ndipo Tid alikamatwa na kuswekwa ndani siku ya Ijumaa na kuachiwa siku ya Jumamosi kwa dhamana na kutakiwa kuripoti kituoni siku ya Jumatatu kwa mahojiano zaidi,
Tid ametoka mida ya saa tano asubuhi kwa Dhamana na ataripoti tena polici jumatatu.
No comments:
Post a Comment