Geez Mabovu, rapper toka Iringa ambaye alikuwa juu sana
miaka flani na ngoma yake ya ‘Mtoto wa Kiume’ na nyingine ameonesha
kutoridhishwa na sapoti anayopewa na media za Tanzania kiasi cha kuhoji
kama kuna mtu amemkwaza amwambie ili amuembe radhi.
Akiongea na tovuti ya Times Fm, Geez amesema anafanya kazi nzuri na kisha kuzisambaza lakini matokeo yake hapati sapoti ya kutosha na hafahamu tatizo hasa ni nini.
“Watu nawatumia na zinafika, ila tatizo ni moja tu…sijui tatizo gani, ni moja nahisi, lakini hilo tatizo mimi binafsi silijui. Kama kazi napeleka, nafanya kazi na nakubali mimi mwenyewe kwamba ni nzuri. Lakini ikifika dakika za mwisho inakuwa haisongi!
“Sasa naona dah! Hivi mimi namakosa gani na hawa jamaa, labda kuna jamaa namkosea? Kama nimemkosea mtu ama nilimkwaza pembeni angeniambia ili niweze kumuomba msamaha, coz sina kawaida ya kugombana na mtu yoyote wala kumwambia mtu maneno machafu wakati sina beef naye. So hiyo kitu huwa inanikwaza na inanivuruga kabisa akili.”Mabovu amefunguka.
Hata hivyo mtoto wa Doll South hakatishwi tamaa na sapoti ndogo anayoipata kwa kulinganisha na kipindi cha nyuma, anaendelea kufanya kazi na kuzisambaza kwa kuwa hajaambiwa kama amemkosea mtu.
“No regret in Life, siwezi kutubu wakati sina madhambi. Kwa hiyo ni bora uniambie kuwa mimi nimekufanyia dhambi hii ili nitubu kwako kwa sababu sipendi ugomvi na siwezi ugomvi. Na ugomvi wangu mimi sijui mwenyewe itakuwaje ikiwa ntawahi kugombana na nyie sijui mtatangaza vipi. Ila sielewi…sielewi, ila mimi naamini nafanya kazi nzuri.”
Geez Mabovu ameachia wimbo wake mpya hivi karibuni unaoitwa ‘Hapa Mpaka Kule’ akiwa amemshirikisha AY, Profesa Jay na Karaban, na umetayarishwa na Lamar katika studio za Fish Crab.

source Timesfmtz.com
No comments:
Post a Comment