Tarajia ngoma mpya ya Darassa na Young Killer. Wawiili hao wameingia ndani ya studio za AM Records kurekodi ngoma iitwayo ‘Usikariri’.
Young Killer ameiambia Bongo5 kuwa ameendelea kutimiza ndoto zake na kufanya ngoma na wasanii wa hip hop aliokuwa akiwakubali na kuwasikiliza.
“Kufanya wimbo na Darassa kwenye muziki wangu ni kuendelea kutimiza ndoto zangu,” amesema Killer. “Hakuna mtu asiyemjua Darassa kwa ngoma zake. Hakuna ngoma ambayo ametoa ukasema hii haiko poa. Utunzi wake ni wa tofauti sana. Kwahiyo kwenye muziki wangu hii ni safari nyingine ya kuendelea kuandika historia baada ya kufanya wimbo na Fid Q, sasa hivi Darassa ingawa amenishirikisha lakini kwangu ni jambo kubwa sana kwa sababu hata mimi nilikuwa nafikiria kufanya naye wimbo,” ameongeza Young Killer.
No comments:
Post a Comment