Tunda Man amesema mashabiki wake wakae mkao wa kula kungojea video yake mpya aliyoshoot nchini Afrika Kusini chini ya muongozaji, Abby Kazi.
Tunda amesema video hiyo ipo kwenye hatua za mwisho za editing.
“Nashukuru mungu tour yangu ya South Africa ilikuwa poa sana, nimeenda salama nimerudi salama,” ameiambia Bongo5. “Kule Nimefanikiwa kufanya video mpya na Abby. Nilimchukua Abby ili awe mwongozaji kwa sababu kampuni ambayo tumetumia vifaa vyao hawajui kiswahili, kwahiyo Abby amesimama kama director na hiyo kampuni tumetumia vifaa vyao. Hii Video itatoka soon, kwa sababu kila kitu kinaenda vizuri na mwezi ujao katikati ngoma itatoka.”
No comments:
Post a Comment