Monday, November 10, 2014

BALOZI WA GHETTO RADIO AWACHAMBA WASIOTOA KWA JAMII

Balozi wa kituo cha redio mpya jijini bongo, Juma Nature juzi amewajia juu wale ambao hutumia fedha zao katika mambo ya anasa na kuisahau jamii na matatizo yake.
Balozi wa Ghetto Radio Sir, Juma Nature akitandika moja ya mashuka yalitolewa sapoti kwa Hospitali ya Temeke na Ghetto Radio.
Nature ambae ni mwanamuziki wa bongofleva toka Temeke alilonga hayo alipokuwa akifafanua jambo mbele ya waandishi na kutoa mfano wa msaada wa kijamii uliotolewa na kituo cha redio cha Ghetto fm kwa hospitali ya Temeke jijini Dar, kwamba mabo kama hayo ndo jamii inatakiwa kuyapa kipaumbele na sio bata na starehe zisizokuwa na msingi.

Mengi ya haya sikiliza Ghetto radio kupitia 94.5fm Dar au ingia online kupitia www.ghettoradio.co.tz upate utamu na wadau wa Jamvini mida ya tatu kamili asubuhi.
Balozi Nature akiwa na timu ya wafanyakazi wa Ghetto walipokwenda kutoa sapoti Hospitali ya Temeke juzi.

No comments: