Wednesday, November 5, 2014

Beyonce aongoza orodha ya Forbes ya wanawake kwenye muziki walioingiza fedha nyingi zaidi 2014

Beyonce ndiye mwanamke kwenye muziki aliyeingiza fedha nyingi zaidi mwaka 2014.
beyonce
Kwa mujibu wa jarida la Forbes, mke huyo wa Jay Z ameingiza dola milioni 115 mwaka huu ikiwa ni zaidi ya nusu ya aliyoingiza mwaka jana. Fedha hizo zimepatikana zaidi kutokana na ziara yake ya muziki duniani na hivyo kumpiku Taylor Swift ambaye mwaka huu amekamata nafasi ya pili kwa kuingiza dola milioni 64.

Pink amepanda kutoka nafasi ya nane mwaka jana hadi kukamatana nafasi ya tatu kwa kuingiza $52 million. Rihanna amekamata nafasi ya nne kwa kuingiza $48 million na Katy Perry ya tano akiingiza $40 million.
Wengini ni:
6.Jennifer Lopez – $37 million
7.Miley Cyrus ($36 million, tie)
8.Celine Dion ($36 million, tie)
9.Lady Gaga ($33 million)
10.Britney Spears ($20 million)

No comments: