Msanii huyo wa kizazi kipya aliewahi kufanya vizuri kimuziki katika ku-rap na hata kuwa mmoja wa wasanii wa kwanza kuanzisha show za luningani maarufu kama ‘reality show’ inasemekana eti alifanya vituko mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kutishia kuwapa yale makonde yake mazito wale wadaku wa habari waliojazana mahakamani hapo ili kuchukua matukio muhimu ya muendelezo wa picha lake ambalo wadau bado hawajalipa jina.
Sambamba na mikwara hiyo, msanii huyu ‘bondia’ wa uzito usiopimwa ambae ni mkazi wa maeneo ya maghorofani ilala alifurumusha matusi ya nguoni kwa wambea hao wa habari bila kujali mahali alipo wala kesi inayomkabili mbele yake, hali iliyosababisha kamera za wambea hao kufanya kazi mara mbili zaidi ya kawaida ilimuradi tu mori ya jamaa huyo izidi kupanda na kuharibu zaidi.
Nje ya kituko hicho, msanii wetu huyu’kioo cha jamii’ akapata wakati mwingine mgumu, huku mwanga wa kamera ukimchanganya, ikatokea hili nalo, akazuiwa kuingia ndani ya chumba cha Mahakama na baadhi ya askari, kisa!?, mavazi aliyokuwa amevaa yakiwemo mapambo.
Mzee mzima huyo alitinga mahakamani hapo akiwa ameji ‘pimp’ na cheni kadhaa shingoni, kipini, huku akiwa na mlegezo mmoja hatari, hivyo mmoja wa askari kumtaka jamaa afunge vifungo vya shati, kupunguza mapambo na kupandisha suruali yaake, duh!
Baada ya kutii onyo hilo, Chid Benzi ndipo aliruhusiwa kuingia mahakamani mbele ya Hakimu Mkazi Warialwande Lema pamoja na jopo la mawakili wawili likiongozwa na wakili wa serikali Ofmed Mtenga akishirikiana na Leornad Challo.
Wakili Mtenga alidai, kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, hivyo wanaomba tarehe nyingine ya kutajwa.
Baada ya Mtenga kudai hivyo, Hakimu Lema alihairisha kesi hiyo hadi Desemba 1. Rapa huyo mgomvi yupo nje kwa dhamana ya wadhamini wawili wa kuaminika waliosaini bondi ya sh.milioni moja kwa kila mmoja.
No comments:
Post a Comment