Hamilton alifanikiwa kutwaa ubingwa huo baada ya kumaliza mbele ya Felipe Massa toka Brazil na Valteri Boltas wa Finland.
Hamilton anamaliza kwenye msimamo wa madereva akiwa amejikusanyia jumla ya pointi 384 akiwa amemzidi mwenzie toka timu ya Mercedes Mjerumani Nico Rosberg kwa pointi 67 .
Hamilton na Rosberg wamekuwa na upinzani mkubwa tangu kuanza kwa msimu huu ambapo wamegawana mara ambazo kila mmoja ameongoza msimamo wa madereva huku kwa karibu msimu mzima ukiongozwa na madereva hao toka Mercedes .
Bingwa mtetezi kabla ya kutwaa kwa Lewis Hamilton Mjerumani Sebastian Vettel ambaye juzi alitangazwa rasmi kuwa dereva mpya wa timu ya Ferarri alikuwa na msimu mbaya ambapo amemaliza kwenye nafasi ya tano katika msimu ambao ameshindwa kushinda mbio hata moja .
Ushindi huu unamfanya Hamilton kuweka Historia ya kuwa dereva wa nne toka Uingereza kushind aubingwa wa Formula one mara zaidi ya moja na kuendelea kuweka rekodi nyingine kama Muingereza aliyeshinda mbio nyingi ndani ya msimu mmoja akiwa ameshinda jumla ya mbio kumi na Mbili .
No comments:
Post a Comment