Saturday, November 8, 2014

Jose Chameleone agoma kutumbuiza kwenye show ya Davido ya Dec. 6 Uganda, Hii ndio sababu

Mfalme wa muziki wa Uganda Dr. Jose Chameleone mwanzoni mwa mwaka huu alitoa collabo yake na star wa Nigeria David Adedeji Adeleke a.k.a Davido, wimbo unaoitwa “All di girls”. Lakini mashabiki wa wasanii hao hawatapata nafasi ya kushuhudia mafahari hao wawili wa Afrika wakiutumbuiza wimbo huo pamoja kwenye show ya Davido iliyopangwa kufanyika December 6, 2014 nchini Uganda.
Davido-Chameleone
Kwa mujibu wa mtandao wa Big Eye, inadaiwa kuwa waandaaji wameshindwa kufikia kiwango ambacho Chameleone ametaka kulipwa ili atumbuize na Davido ambacho ni US $ 3000, yes sijakosea ni US $ 3000 (sawa na zaidi ya Tsh milioni 5).

No comments: