Ingawa tetesi za kitaa zinavuma kwamba msanii huyo babu katika anga lamuziki wa Bongo fleva amekufa kisanii na ni ngumu kulipanda tena jukwaa hili la sanaa, Nature mwenyewe ana muono tofauti sana na hilo na kuamini kwamba shujaa hafi bali hufifia na muda si muda hurejea.
“Mashujaa hawapotei hivyo ndivyo historia inavyohukumu, wao hufifia na punde huweza kurejea, nafasi ya ubalozi ni silaha njema kwangu na kwa washkaji wa ghetto”, anena Nature.
Imani ya wana Ghetto Radio ni kwamba Sir Juma Nature ‘Kibla’ ni kwamba ataiwakilisha vyema Redio hii na kufanya yale yalio vichwani mwao kwani Nature, ni alama tosha kwa walengwa wa wa Ghetto Radio, ambao ni jamii ya tabaka la kati na chini ila hususani vijana wa miji mikubwa kama Bongo.Imani hii inakuja pale ambapo msanii huyu kuwa ni mmoja wa wale vijana waliokulia na kuishi uswahilini ambako ndiko maarufu kwa vijana wa ghetto, hivyo Nature ni jina sahihi kama balozi wa kwanza kwa kituo hiki kipya Bongo.

Utamu ulikuja pale msanii huyo alipopata nafasi ya kutembelea studio ya kisasa ya Ghetto FM maeneo ya kinondoni na kufanya tour ndogo ya maeneo yote ndani ya ofisi hizo, ambapo Sir Kibla alikutana na baadhi ya wafanyakazi na kupiga nao stori za hapa na pale, huku akiwarusha na kukanyagana ndani ya studio kwa nyimbo zilizovuma kitambo kile na hata sasa kama vile, Jinsi kijana,Hakuna kulala, Sonia, ndege tunduni, huku akiwalisha ugali wa Kighetto ghetto .
Ghetto FM Radio inatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe mosi Novemba mwaka huu saa sita usiku huku ikifuatiwa na mlolongo mreefu wa matukio ya misaada kwa jamii kwa hospitali ya wilaya ya Temeke, ubandikaji wa stika kwenye bodaboda na bajaji na utambulisho rasmi wa vipindi na wafanyakazi wa Ghetto Radio ya Sibuka FM.
No comments:
Post a Comment