Aliitika wito wa Mkasi TV, na tulipata wasaa wa kipekee kuzungumza nae. Akiwa binti mchanga kabisa wa miaka 20, mengi yaliyosikika kutoa kwake yalionesha upeo na ukomavu wa kiakili. Lakini zaidi, yalithibitisha kuwa mtoto anapokulia kwenye mazingira yenye upeo, na hukua kiakili mapema.
Happy ni mmoja kati wa vijana wa Kitanzania waliopata nafasi za kusoma na kuhitimu katika shule moja ya Kitamaifa nchini, na katika masomo yake kuna mafanikio mengi, moja likiwa kuwa mmoja kati ya wanafunzi waliofanya vema sana kwenye somo la Uhasibu, katika mtandao wa Shule za Sekondari za Kimataifa. Mahiri kwenye lugha, na akiwa na historia ya kutembelea nchi mbali mbali, ni dhahiri huyu ni Miss Tanzania wa kipekee.
Akiwa ana matarajio ya kuendelea na masomo endapo hatofanikiwa kutwaa taji la Miss World, Bi. Happy anabeba bendera ya Tanzania kwa matumaini makubwa ya kuliwakilisha taifa vema. Taifa nalo lina nafasi na wajibu wake kumpa sapoti anayohitaji kufanya vema.
No comments:
Post a Comment