Shirikisho la soka nchini TFF, linakaribisha wabunifu, kubuni mwonekano wa jezi mpya za timu ya Taifa kwa mechi za nyumbani na ugenini. Ubunifu ni lazima uzingatie rangi za bendera ya Taifa.
Mshindi wa jezi ya nyumbani atapata sh. 1,000,000 (milioni moja), na mshindi wa jezi ya ugenini atapata pia sh. 1,000,000 (milioni moja).
Ubunifu utumwe kwenye anwani ya barua pepe: info@tff.or.tz au uwasilishwe kwa CD au flash zikiwa katika mfumo wa PDF katika ofisi za TFF zilizopo ghorofa ya tatu katika Jengo la PPF Tower, Mtaa wa Ohio na Garden Avenue. Mwisho wa kupokea designs ni Novemba 15, 2014.
Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba; 0713 210242 au 0714 634838.
Wakati huo huo Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewatumia salamu za rambirambi vyama vya mpira wa miguu vya Zambia (FAZ) na Afrika Kusini (SAFA) kutokana na vifo vya Rais Michael Sata na kipa wa timu ya Taifa ya Afrika Kusini, Senzo Meyiwa.
Ametuma salamu hizo kwa Rais wa FAZ, Kalusha Bwalya na Rais wa SAFA, Danny Jordan na kuongeza kuwa amepokea kwa masikitiko taarifa za vifo vya ghafla vya Rais Sata na kipa huyo wa Bafana Bafana vilivyotokea wiki hii.
Rais Malinzi amesema kuwa misiba hiyo si pigo kwa Zambia na Afrika Kusini pekee bali Afrika kwa ujumla kwa vile walikuwa na mchango mkubwa kwa ustawi wa mchezo wa mpira wa miguu.
Amewaomba Rais Jordan na Rais Bwalya kutuma salamu zake za rambirambi kwa familia ya Sata, na familia ya Meyiwa, na kuzitaka kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha misiba hiyo mizito kwao.
Rais Sata (77) alifariki dunia juzi kwenye Hospitali ya King Edward VII nchini Uingereza alipkuwa kwenye matibabu, wakati kipa Meyiwa aliuawa kwa kupigwa risasi Jumapili mjini Voslooru
No comments:
Post a Comment