Monday, November 10, 2014

Walichokifanya Watanzania Vanessa, Shaa, Diamond na Joh Makini kwenye fainali ya #CokeStudioAfrica

Screen Shot 2014-11-10 at 1.08.02 PM Nimekuja kujikuta #CokeStudioAfrica ni show nyingine ninayopenda kuitazama kwenye TV ikiwa na muunganiko wa Wasanii wakali wa Afrika ambao wanatuteka kwa kufanya nyimbo zao live pamoja.


Kwenye hii fainali ambayo ilifanyika Jumamosi November 8 2014 Mtanzania Vanessa Mdee alimiliki stage akiwa na Burna Boy wa Nigeria, Joh Makini na Chidinma wa Nigeria, Diamond Platnumz na Yemi Alade wa Nigeria na Shaa ametokea kwenye single ya Wyclef Jean.
Shaa ndio Mtanzania pekee ambae hajaonekana kwenye hizo video 3 hapo juu, taarifa ikufikie kwamba yuko kwenye hii hapa chini akiwa na mkali Wyclef Jean.
Baada ya kutazama zote hizi nitaomba uniachie comment yako mtu wangu nini umekifurahia sana kwenye hizi video?

No comments: