Aliyekuwa mume wa mwanamuziki wa Injili Flora Mbasha, Emmanuel Mbasa
ambaye nae pia ni mwanamuziki wa Injili nchini Tanzania amefutiwa
mashtaka ya kesi iliyokuwa ikimkabili Mahakama ya Ilala, Dar ilimwacha
huru Emmanuel Mbasha Hapo Jana Jumatatu Septemba 21, 2015 baada ya
upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha kosa la ubakaji dhidi yake.

Itakumbukwa mwaka 2014 Emmanuel Mbasha ambae ni mwimbaji wa injili na
mfanyabiashara alifunguliwa mashataka mawili mahakama ya Ilala kwa
makosa mawili ikiwemo la ubakaji. Katika shtaka la kwanza Mei 23, mwaka
2014 eneo la Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam,
ilidaiwa kinyume cha sheria alimuingilia kwa nguvu msichana anayedaiwa
kuwa shemeji yake. Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Mei 25, mwaka
2014 eneo la Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria,
mshtakiwa alimuingilia kwa nguvu mfanyakazi wake.
No comments:
Post a Comment