Thursday, November 26, 2015

Vanessa aelezea kwanini amechelewa kuachia album yake ‘Monday Mondays’

Muimbaji wa ‘Never Ever’ Vanessa Mdee ameelezea sababu za kwanini album yake mpya ‘Monday Mondays’ imechelewa kutoka.
12276907_984236138289678_255207204_n
“Naichelewesha kuitoa sababu natafuta proper distribution plan,” Vanessa Mdee ameiambia Djjonamusic Blog

“Sitaki tu itoke halafu watu wakasikiliza halafu ikabakia hamna faida yoyote tuliyotengeneza. Nataka kutumia fursa kutengeneza album ambayo italeta utofauti kwenye utoaji wa album. Kwasababu kwenye masuala ya muziki tuko vizuri lakini tunasambazaje? Je tukisambaza tunategemea kupata faida gani?, tuna make sure vipi inafika kote kule inakotakiwa kufika?, Kwahiyo hivyo ni vitu ambavyo navifanyia kazi kabla sijaitoa,” ameongeza.
Hata hivyo amesema kuwa Tayari album hiyo imekamilika na itatoka hivi karibuni.

No comments: