Sunday, January 10, 2016

Mashabiki Wanataka Kuendesha Muziki Kitu Ambacho Sio Sawa – Mwana FA

Mwana FA amewataka mashabiki wa muziki nchini kuacha tabia ya kuwalazimisha wasanii wa muziki kufanya kila kitu wanachokitaka hata kikiwa hakina mantiki kwa wakati huo.
Rapa huyo aliyeachia video ya wimbo ‘Asante kwa Kuja’, amekiambia kipindi cha 360 kinachoruka Clouds TV kuwa msanii ndiye anayetakiwa kumbadilisha shabiki kwa kumpatia vitu tofauti. “Mashabiki wanataka 

kuendesha muziki kitu ambacho sio sawa na sio sahihi,” alisema FA.
“Ukienda kule kwenye page za Instagram ambako mashabiki wanaweza kukufikia kiurahisi unaweza ukapata lawama kwanini haubadiliki una sound kama old school rapa au mwingine anataka ubaki kama ulivyokuwa unarap zamani bila kujua sasa hivi tupo mbele zaidi.”
“Muziki sio kama ni jiwe tuuchukulie kama mti unakuwa na kuna changes zinatokea. Lazima tubadilike ukiangalia video zangu sidhani kama unataka nifanye tena video kama ya ‘Mabinti’. So ni lazima watu wakue, dunia inaenda kasi na muziki unakuwa ni lazima ubadilike. Kwahiyo mtu akiniamba hataki nibadilike anataka nibaki nilivyokuwa, sielewi,” alisisitizia FA.

No comments: