Msanii wa muziki wa Hip Hop Nay wa Mitego
amesema hakupenda ujauzito wa Wema Sepetu uharibike kama baadhi ya
mashabiki wa Wema Sepetu wanavyodai katika mitandao ya kijamii. Rapa
huyo kupitia wimbo wake “Shika Adabu Yako’ alimchana Wema ‘una mimba
kweli, au ndio kiki za msimu?. Miezi tisa

sio mingi, isije ikakugharimu”
kauli ambayo ilitafsiriwa vibaya na mashabiki wa Wema.
Akizungumza katika kipindi cha Ubaoni cha EFM Jumatano hii, Nay alisema yeye hawezi mwombea mabaya Wema kwa kuwa anapenda sana watoto.
“Sijapenda ujauzito wa Wema uharibike kwani napenda watoto. Kama ilikuwa mimba kweli nampa pole sana dada yangu ila kama ilikuwa kiki imefika mwisho Kwani nilichoongea kwenye wimbo ilikuwa ni swali Je? Una mimba kweli au drama.,”alisema Nay.

No comments:
Post a Comment