Msanii wa muziki kutoka Tip Top
Connection, Madee amefunguka na kudai kuwa siku zote atamlaumu msanii
wa Bongo flava na aliyewahi kuwa chini ya usimamizi wa Tip Top, Mb Doggy
kwa kuondoka kwenye lebo hiyo. Akizungumza katika kipindi cha Hatua
Tatu cha Times Fm, Madee amedai Mb Dog alikosea
kuondoka Tip Top kwa
kuwa alikuwa chini ya mikono sahihi. “Mimi kitu ambacho nitaendelea
kumlaumu Mb Doggy ni kuondoka Tip Top, unajua unapokuwa kwenye malezi ya
baba na mama mmoja hata maadili ni yale yale, unapoenda sehemu nyingine
unakutana na vitu vipya, alafu si tulikuwa tukitoa nyimbo Babu tale
ndiyo anaenda kushughulika kila kitu kupeleka Radio na vitu vingine,
sasa hakuwa na menejimenti kila kitu alikuwa akifanya yeye baada ya
kutoka nahisi ndiyo maana akashindwa” Alisema. Kwa sasa MB Dog yupo
chini ya label ya QS Mhonda Entertainment pamoja na Q Chief. Ambapo
mpaka sasa ameshaachia kazi kadhaa, moja wapo ni video ya wimbo ‘Sio
Siri’ ambayo ulifanya vizuri.
No comments:
Post a Comment