Jacqueline Wolper anaweza kuwa kimya kwenye
filamu kwa kipindi kirefu lakini ana mipango mikubwa kwenye tasnia hiyo.
Muigizaji huyo amedai kuwa na mpango wa kuja na filamu aliyoshirikiana
na ex wake Diamond Platnumz. Wolper ambaye kwa sasa ni mpenzi wake na
Harmonize, alikiambia kipindi cha Take
One cha Clouds TV wiki hii kuwa
pamoja na kwamba aliwahi kuwa na uhusiano na staa huyo na kisha
kuachana, bado wamebaki kuwa washkaji wa nguvu. Alisema ukaribu wao ni
zaidi ya urafiki na wameendelea kushirikiana katika mengi. Ni kweli
kwakuwa Wolper ndiye ex wa Diamond pekee aliyeonekana kwenye video ya
Utanipenda. Hata hivyo hakusema ni lini filamu hiyo itaanza kufanyiwa
maandalizi. Kama itakuwepo, hiyo itakuwa filamu ya kwanza ya Diamond.
No comments:
Post a Comment