Sunday, June 5, 2016

Diamond Platnumz aongelea suala la Wema kumsupport na mawasiliano yao tangu wameachana

Vita ya mashabiki wa Diamond na Wema tangu wapenzi hao waachane ilikuwa kubwa hadi Wema alipoamua kumsupport mpenzi wake huyo wa zamani kwa post kazi zake kwenye Instagram yake.

Wema alipost kuwaomba watanzania wampigie kura Diamond kwenye tuzo za BET, Pia alipost tena tukio la usajili wa Rich Mavoko kwenye label ya Diamond, WCB.
JESTINA-GEORGE-BLOG 2
“Kuna wakati inafika watu mnakuwa mmekuwa labda, mtu anaona hana sababu ya kuendelea kukuchukia au kuwa na vita na wewe, sababu mwanzo mwanzo mkiwa bado mnaenda mnaona kuna vitu mko navyo ndiyo maana kuna kuwa na chuki kubwa,” Diamond alifunguka kwenye kipindi cha FNL cha Eatv  “Lakini ikifika wakati kila mtu amesonga mbele na maisha yake, ameridhika na maisha yake anaona kwanini nimuwekee vita mtu fulani hivyo nadhani labda wakati huo ndiyo huu maana mwenyewe nimeona kweli amepost BET, amepost promo ya Rich Mavoko kwangu mimi nafurahi kwa sababu naona haina faida kwa sisi wasanii kuwekeana vita”
Alipoulizwa kuhusiana na mawasiliano yao kwasasa, Diamond alisema kuwa hawajawahi kuwasiliana tangu wameachana.

No comments: