Msanii wa muziki wa kisingeli, Amani Khamisi ‘Man Fongo’ amewataka wasanii wa muziki wa bongofleva kupokea ushindani mpya kutoka katika muziki wa kisingeli.
Muimbaji huyo anayefanya vizuri na wimbo ‘Hainaga Ushemeji’ amesema muziki wa kisingeli una nafasi ya kufanya vizuri zaidi kwa kuwa ni muziki wa uswahilini.
“Muziki tunaouimba ni wa mtaani ambapo ndiko chimbuko na watu wa uswahilini, kwa sasa huwaambii kitu kuhusu muziki wetu. Nawaambia ukweli kabisa wasanii wa Bongo Fleva, wakaze buti twende sawa au watafute kitu kingine cha kufanya,” Man Fongo aliliambia gazeti la Mtanzania.
“Ujue wao wanaimba vitu vya kubuni wakati sisi tunaimba maisha halisi hasa ya uswahilini kwa masikini wenzetu,”
Awali watu waliuita muziki wa kihuni kutokana na vijana kufanya matukio mbalimbali ulipokuwa unapigwa kwenye shughuli za mitaani nyakati za usiku maarufu vigodoro.
Pia muimbaji huyo kwa mara ya kwanza amepata shavu la kupanda kwenye jukwaa la Fiesta Mwanza.
No comments:
Post a Comment