Monday, September 26, 2016

Kikwete ahutubia maelfu kwenye tamasha la Global Citizen fest ambalo pia Rihanna, Kendrick Lamar na Usher walitumbuiza

Rais mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete aliungana na maelfu ya kuhudhulia tamasha la Global Citizen fest. lililofanyika New York, Marekani.
IMG_9834

Rais Mstafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Kamishna wa Kamisheni ya Kimataifa kuhusu elimu akizungumza mbele ya umati wa wakazi wa jiji la New York katika tamasha la Global Citizen Festival lililofanyika Central Park. Kupitia tamasha hilo, Mhe.Kikwete aliichagiza jumuiya ya kimataifa kuchangia na kuwekeza katika elimu kwa mustakabali wa kizazi cha sasa na kijacho. Pamoja naye ni Makamishna wenzie, Waziri Mkuu wa Norway Erna Solberg na aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Australia Julia Gillad.
IMG_9855 - Copy

Aidha mapato yaliyopatikana kutoka kwenye tamasha hilo yatatumika kwenye masuala mbalimbali ya kimaendeleo kama Elimu, Miondominu na Afya.

global-citizen-festival-2016
Kwenye Tamasha hilo pia wasanii maarufu wa Marekani, Rihanna, Kendrick Lamar, Usher, Demi lovato na Martin Rock walitumbuiza.

No comments: