Friday, September 9, 2016

Pigo kubwa kwa wafanyakazi wa kings fm radio 104.3 Njombe na Djjonamusic Blog

Cheti cha Pongezi alichokabidhiwa King Dav Na Ofisi ya Kings Fm
Msimamizi Mkuu Idara ya Vipindi katika kituo cha Redio Kings Kilichopo Njombe Mjini David Magobeko(King Dav) ametangaza  rasmi kuacha kazi katika kituo hicho sababu kuu ikielezwa kuwa ni hatua yake ya kubadilisha makazi ya kufanyia kazi.
David Magobeko (King Dav)ni Mwajiriwa wa kwanza katika kampuni ya Kings Broadcasting Services inayomiliki pia kituo hicho cha Redio amabye ni miongoni mwa watu wa karibu waliohusika kukisuka kituo hicho mpaka kuwa na mwonekano wa tofauti kati ya vituo vya Redio Nyanda za Juu Kusini.
Ni jambo jema na lenye kukuongezea furaha na amani pale unapoagana na wafanyakazi na ukiwa umewaacha wakiwa na majonzi yenye furaha katika nyoso zao wakukulilia kuondoka kwako.
Hii inatukumbusha kuwa na mahusiano mazuri  baina ya wafanyakazi mahala pa kazi kwa kufanya kazi kwa upendo,uvumilivu na hasa jitihada zaidi na ufanisi ndio vitu vya muhimu kuzingatiwa.
Hatua ya kutangaza kuacha kazi kwa Bwana Magobeko katika redio hiyo imejiri ikiwa imesalia takribani  miezi mitatu kutimiza miaka miwili Tangu kituo hicho kianze kurusha matangazo rasmi mwishoni mwa Mwaka 2014.
Katika Hafla fupi ya kumuuga Kiongozi huyo ilyofanyika katika ukumbi mdogo wa Agreement Hotel Usiku wa Kuamkia Leo September 9 mbele ya Wafanyakazi Wengine Amesema yeye ni miongoni mwa watu walioishauri bodi ya Wakurugenzi katika kuhakikisha kituo hicho kinakuwa bora zaidi.
Mimi ni muajiriwa wa kwanza Kings fm na mtu ambaye amefanya Kings Fm ikaonekana vile inavyoonekana sasa hivi pale kuanzia kwenye vifaa kwenye kila kitu,sio kwa kununua vifaa ila kwa kushauri bodi ya wakurugenzi ipite kule
Ameongeza kuwa Nilishirikiana na wenye mali kufanya vile amabavyo iko na kupambana kila kilichowezekana kufikisha Kings Fm ilipofikia pale ambapo mpaka leo hii nazungumza nitakuwa nimebakiza kama miezi mitatu ningekuwa nafikisha miaka miwili kamili kuwepo kings Fm,Kwahiyo Too Bad  naondoka sijafikisha miaka miwili,nilikuwa natamani nifikishe miaka miwili nikiwa Kings lakini bahati mbaya imetokea Naondoka Kings
Magobeko amesema kuwa anaamini anakiacha kituo hicho kikiwa kwenye mikono salama.
Akijibu swali lililoulizwa na wafanyakazi  wenzake kama ameacha kazi mwenyewe au amefukuzwa kazi amesema ameacha kazi kwa hiari yake mwenyewe bila kusukumwa na mtu  na ni mambo yake binafsi yalisababisha yeye kuacha kazi ikiwemo sababu ya kubadilisha Makazi.
Imeaminika kuwa Bwana David Magobeko anaenda kujiunga na Timu ya kituo  kimoja cha redio Cha Jijini Dar kinachofanya vizuri na chenye ushindani mkubwa kati ya vituo vingine vya Redio
Hali ya tofauti ilianza kujitokea pale kila mfanyakazi alipopewa nafasi yake kuzungumza na Kingozi huyo ambapo kila mmoja licha ya kufurahishwa na hatua ya kiongozi wao  ya kwenda kufanya kazi mahala pengine lakini wengi wao walijikuta wakipata uchungu na kushindwa kuzuia hisia kwa kububujikwa na machozi kwa masikitiko makubwa walimpongeza kwa kuwa kiongozi bora aliyefanya kazi kwa kutenda haki bila kujali makundi.
Hata Hivyo Afisa Masoko wa Kings Fm Abel Mponela licha ya kumtakiwa mafanikio mema huko anakoenda amemuomba asisite kushirikiana na wafanyakazi wanaobaki katika kituo hicho hasa katika kutoa ushauri na matumizi ya Teknolijia mpya zinazoenda na wakati kwa lengo la kuboresha huduma ya matangazo ya redio.
Hafla hiyo ilifungwa na Kaimu Meneja wa Kituo Hicho Emilia Msafiri akimpongeza kwa kuonyesha ushirikiano wa hali na mali akiwa kama kiongozi na mwisho alimkabidhi Cheti cha Shukrani.
Hapa Chini ni Baadhi ya Picha za wafanyakazi wa Kings Fm
 
Kushoto ni Emilia Msafiri Kaimu Meneja Kings Fm na King Dav
 
Kushoto ni King Dav na Erasto Mgeni Mhariri Mwandamizi Kings Fm
King Dav Akiwa na Afisa Masoko Abeli Mponela Kulia
King Dav Akiwa na Skawa Juniour mtangazaji wa Kipindi cha Kings Drive 
King Dav Akiwa na Kaizar Bravo wa Kambi ya Sport
King Dav Akiwa Pili Nyenje Mama Nyeupe wa African Vibe
King Dav akiwa na Ramalove wa Super Mega
King Dav akiwa na Comedian Copo anasikika kwenye Fire Beat
King Dav akiwa na Producer wa Kings Fm Brian Davis Briz
Anaye kata Keki ni Nana Jacob wa Kings Drive
King Dav Akiwa na Mwinyi Mwinyi wa Kambi ya Sport
King Dav Akiwa na Nana Jacob, Teresia Alex wa Kachumbari   wa katikati 
SOURCE  WEBSITE YA KINGS FM RADIO

No comments: