Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama
Salma Kikwete amewaasa wasanii wawili wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba
na mdogo wake Abdu Kiba kuwa wawe waaminifu kwenye maisha yao ya ndoa
hasa hasa kwenye masuala ya simu.
Mama Salma ametoa wosia huo jana Aprili 29, 2018 katika hoteli ya
Serena jijini Dar es salaam kwenye sherehe za harusi ya Alikiba na
mdogo wake Abdukiba ambao wote wamefunga ndoa wiki mbili zilizopita.
“Simu mtihani na ni hatari, mkiendekeza simu mnachukua
mnaangalia mtaaachana kabla ya siku si nyingi. Aminianeni mkiaminiana
maisha yatakuwa mazuri, laikini kila dakika ukirudi basi umerudi unaanza
kupakua nani ametuma meseji, hapana. Wakati mwingine simu inalia
ikishalia ile simu unakosa amani ya moyo unatoka nje au unaingia chooni
kuongea,“amesema Mama Salma Kikwete.
Kwa upande mwingine Mama Salma Kikwete amesema yeye tangu afunge ndoa
na Mzee Kikwete wamekuwa wakichangia simu na mara nyingine hata
kupokeleana pale inapokuwa inaita.
Alikiba na mdogo wake Abdukiba wamefunga ndoa wiki mbili zilizopita
ambapo Alikiba alifunga ndoa na mchumba wake Aminah Khalef jijini
Mombasa.
No comments:
Post a Comment