Baba ndogo wa mwanamuziki wa Hip Hop, Godzillah aliyefariki dunia leo
Jumatano Februari 13, 2019 amesema ndugu yake aliteswa na kitu
kilichokwama tumboni kwa zaidi ya siku tatu na kumfanya atapike
mfululizo.
Akizungumza leo nyumbani kwao Salasala jijini Dar es Salaam, Joyce amesema mwanamuziki huyo Golden Mbunda alikuwa akitapika kwa siku tatu mfululizo.
Amesema rapa huyo aliyewahi kutamba na wimbo Lakuchumpa alianza kujisikia vibaya na alipokwenda hospitali alibainika kuwa na malaria, sukari kuwa juu na presha.
“Jumapili (Februari 10, 2019) alilala muda mrefu, haikuwa kawaida. Baadaye akaomba barafu tulivyompa akaanza kutapika ndipo tulipompeleka hospitali na kugundulika ana malaria, sukari imepanda sana na presha imeshuka,” amesema.
“Pia marehemu alisema kuna kitu kiling’ang’ania tumboni kama vile kinataka kutoka ila kinagoma, alijaribu kukitoa kwa kujitapisha lakini hakikutoka.
No comments:
Post a Comment