Shirikisho la soka Afrika CAF kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo nguli Afrika Mamadou Gaye, CAF wametengua uteuzi wa Didier Drogba kama mshauri wa Rais wa CAF Ahmad Ahmad.
July 2019 staa wa zamani wa Chelsea na Ivory Coast Didier Drogba na staa wa zamani wa Barcelona na Cameroon Samwel Eto’o waliteuliwa kuwa washauri wa Ahmad Ahmad lakini Drogba hajafanya chochote toka uteuzi huo utangazwe.
Drogba na CAF bado hawajathibitisha taarifa hizo lakini zimeenda mbali zaidi kwa kueleza Drogba toka ateuliwe hajawahi kushauri chochote kama majukumu yake yanavyotaka lakini pia hajawahi kuhudhuri shughuli yoyote ya CAF ikiwemo mechi hata moja ya AFCON 2019.
Chanzo;millardayo.com
No comments:
Post a Comment