Mchezaji wa zamani wa Juventus Alessandro del Piero anaamnini Guardiola atakuwa ‘kiungo muhimu’ katika klabu hiyo. Meneja huyo wa City ahusishwa na tetesi za kuchukua nafasi ya Maurizio Sarri mjini Turin. (Sky Sports)
Wakala wa winga wa Manchester City Raheem Sterling amesema kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 25 amejitolea kuhudumia” klabu hiyo na kwamba “hatashawishiwa na mazungumzo yoyote ya uhamisho kutoka klabu hiyo kwa sasa”. (Mirror)
Manchester City Raheem Sterling hana mpango wa kuondoka Manchester City
Manchester City imethibitisha kuwa baadhi ya wachezaji wake wanataka kuondoka mwisho wa msimu huu ikiwa marufuku dhidi ya kushiriki Champions League itadumishwa. (Telegraph)
Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer haamini kuwa wakishindwa kujikatia tiketi ya kushiriki Champions League kutaathiri mpango wa uhamisho wa klabu hiyo. (Mirror)
Solskjaer anasema uhamisho wa mkopo wa mshambuliaji wa Nigeria wa miaka 30, Odion Ighalo kuja Manchester United kutoka Shanghai Shenhua huenda ukafanywa wa kudumu. (Manchester Evening News)
Uhamisho wa mkopo wa mshambuliaji wa Nigeria wa miaka 30, Odion Ighalo kuja Manchester United huenda ukafanywa wa kudumu
Barcelona italazimika kumjumuisha mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann katika mpango wowote utakaojaribu kuishawishi Inter Milan kuwauzia Lautaro Martinez. (Sun)
RB Leipzig inasisistiza kuwa Liverpool haijawasiliana nayo kuhusu mshambuliaji wake Timo Werner. Kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 23, amefunga mabao 20 katika ligi kuu ya Bundesliga msimu huu. (Mirror)
RB Leipzig inasisistiza kuwa Liverpool haijawasiliana nayo kuhusu mshambuliaji wake Timo Werner.
Mchezaji Gabriel Magalhaes, ambaye yuko klabu ya Ufaransa ya Lille na anayenyatiwa na Arsenal, anasema “agelipendelea” kucheza katika ligi ya Premia. Beki huyo wa Brazil wa miaka, 22, pia analengwa na Everton. (Sun)
Inter Milan inajadiliana na Manchester United kuhusu usajili wa mchezaji kinda Tahith Chong. Mkataba wa Winga huyo wa miaka 20 Old Trafford unakamilika msimu huu wa joto. (Tuttosport, via Sun)
No comments:
Post a Comment