Afisa Habari na Mhamasisha wa Mabingwa wa Kihistoria wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara Young Africans, Antonio Nugaz amewahamasisha mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi siku ya Jumapili kuishangilia timu yao huku akiongea kwa msisitizo mkubwa kuwa ‘Bila Makandokando’ Wanajangwani hao hawawezi kufungwa.
”Wape salamu Kuwa Jumapili tunakutana nao tukiwa tuko Sawa. Mwana Yanga tembea ringa tena Vimba, jitambe Sisi bila Makando kando hatufungwi. Timu yetu ndiyo iliyojenga historia ya Nchi hii”- Afisa Mhamasishaji wa Young Africans Antonio Nugaz akifunguka kuelekea mchezo wao wa Watani wa Jadi dhidi ya Mnyama Simba siku ya Jumapili ya tarehe 8/03/2020
No comments:
Post a Comment