Saturday, March 14, 2020

Hudson- Odoi wa Chelsea athibitisha kupona Corona (+Video)

Callum Hudson-Odoi akiwa mchezaji wa kwanza kunako Premier League kugundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona, hatimaye hii leo siku ya Ijumaa kupitia kipande cha video amethibitisha kupona ugonjwa huo nakudfai kuwa muda si mrefu wapenzi wasoka watarajie kumuona tena uwanjani.

 

Mapema asubuhi Ijumaa, Chelsea ilitanga kuwa winga wake huyo alionyesha kuwa na dalili za virusi vya Corona siku ya Jumatatu. Na hivyo kikosi chote cha kwanza pamoja na baadhi ya wafanyakazi waliokuwa karibu na Hudson-Odoi walilazimika kutengwa.
Image result for Hudson- Odoi
Akizungumza hadharani kwa mara ya kwanza tangu kutangazwa kuwa na virusi vya corona, Hudson-Odoi afya yake imeimarika na anatarajia kurejea baada ya kuumwa katika siku kadhaa.
‘’Habari zenu, kama mlivyoweza kufahamu kuwa nilikuwa na virusi siku kadhaa zilizopita, ambapo nimepona,” Hudson-Odoi amesema kupitia kipande cha video.
‘’Nafuata miongozo ya afya na kujitenga na kila mtu kwa wiki. Natumaini kuona kila mtu hivi karibuni na matumaini yangu ni kurejea uwanjani hivi karibuni.”

No comments: