Kwa longtime sasa hivi
Tanzania imeshuhudia magazeti mengi pamoja na stori za internet kwenye
blogs, website na facebook kuhusu Freemasons, kwa kiasi kikubwa baada
ya hizo habari, picha iliyojengeka kuhusu Freemasons ni kwamba ni dini
ya kishetani.
Wametajwa mastaa
mbalimbali wa Tanzania pamoja na viongozi wa kisiasa kwamba nao
wamejiunga na dini hiyo akiwemo rais mstaafu wa Tanzania William Mkapa
na Rais Mwai Kibaki wa Kenya.
Exclusive kwenye THE
INTERVIEW ya CLOUDS TV Mtangazaji Gerald Hando amefanya interview na
Sir Andy Chande ambae alikua freemasons lakini kwa sasa amestaafu.
Moja kati ya mambo
aliyoyazungumzia ni pamoja na taarifa za Kibaki na Mkapa kuwemo kwenye
hicho chama, hapa namkariri akisema “Hakuna hata mmoja kati ya mkapa
wala kibaki ambae ni Freemason, nilipofika hapa mwaka 1950 katika
biashara zangu nilikutana na watu wengi katika Nyanja mbalimbali ambao
walikuwa wakiandaa chama cha freemasons ambao walinialika kwenye vikao
mbalimbali Uganda, Kenya, uingereza na kwingineko kama Ghana na Khumasi
ila nikastafu baada ya miaka 19 kufanya kazi na freemasons.
Sihusiki tena na
freemasons huku Tanzania, ila kama uingereza naenda mara kwa mara kwa
sababu bado kuna baadhi ya mashirika ninayofanyakazi nayo hadi sasa,
Freemasons sio kama watu wengi wanavyosikia au kuambiwa.. kuna tofauti” .............posted by deejay jona
No comments:
Post a Comment