Ukifuatilia Tweet Page za Kanumba na Elizabeth
Michael aka Lulu utaona kuwa walijaribu kutumia majina ya Mopao na Cindy
labda kunogesha chat yao au katika kupoteza maboya wafuasi wao kwenye
mtandao huo wa kijamii au labda kujifananisha na nguli ambaye Kanumba
mwenyewe aliwahi kukiri kuwa anampenda sana Koffi Charles Olomide Mopao
Sakonzy, huku Kanumba akimuita Lulu Cindy na Lulu akimuita Kanumba
Mopao.
Kanumba alikuwa mpenzi mkubwa sana wa Bolingo na jina la Mopao ni jina la Koffi Olomide
ambaye mashabiki wanamuita Mopao Mokonzi. Koffi amekuwa kwenye uhusiano
wa kimapaenzi na muimbaji wake wa kike anayejulikana kwa jina la Cindy Le Coeur
ambaye kwa sasa ndiye mke wake kipenzi. Koffi wakati akiaanza uhusiano
na Cindy ilikuwa ni siri na iliandikwa sana kwenye vyombo vya habari
lakini kila mara walipoulizwa walikana mpaka kwenye Birthday ya Cindy
ndipo Koffi alipovunja ukimya na pale alipomzawadia gari aina ya Jaguar
baba yake na Cindy (Gonga hapa kuisoma)
na mpaka wa leo Cindy ambaye anakuja kwa kasi kwenye wanamuziki wa kike
na amejizolea umaarufu kwa nyimbo zake za Koffi Chante Cindy ambapo
amekuwa akizirudia nyimbo za taratibu za Koffi tangu enzi hizo.
Sasa baada ya kukueleza hayo soma Tweet za mwisho za Kanumba “Mopao” na Lulu “Cindy”.





Compilation ya Tweet hizi ni kwa hisani ya Shafi Dauda Blog.
No comments:
Post a Comment