Saturday, September 8, 2012

KAULI YA KWANZA YA DANIEL AKUFFOR WA SIMBA BAADA YA KUZIMIA UWANJANI JUZI.

kwenye mechi na Sofapaka ya Kenya juzi september 6 2012, mchezaji wa Simba Daniel Akuffor amesema kwa sasa anaendelea vizuri na ataendelea kuwa fit kadri siku zinavyosogea.
Akuffor amesema “sijui nini kilitokea kwa sababu hii ni mara yangu ya kwanza kwenye maisha yangu miaka 12 kwenye soka sijawahi kupatwa na kitu kama hiki, niko poa na niko tayari kwa game ijayo ya ngao ya jamii na ushindi utapatikana”
Kwenye line ya mwisho Akuffor amewaambia fans wa Simba kwamba wasiwe na wasiwasi na hadhani kama kilichotokea kwenye mechi ya Simba na Sofapaka kitajirudia.

No comments: