Thursday, September 6, 2012

MASTAA WA KIKE 5,WALIOWAHI KUBAKWA UTOTONI.

 
1 Mary J Blige.
Mary J Blige ni moja ya wasanii wakubwa wa kike ambaye aliwahi kukiri kubakwa akiwa mtoto.Mary J Blige mwenye umri wa takribani miaka 41 hivi sasa, alisema kuwa akiwa na miaka 5 alibakwa na mmoja wa marafiki wa familia. 
 Mary J.
Msanii huyo wa kike mwenye tuzo 9 za Gramy alisema kuwa kitendo hicho kilimuathiri nakumfanya akue akiwa anajutia, ajione hana thamani na maumivu na hata kujiingiza katika mapenzi na wanaume tofauti tofauti na madawa ya kulevya.Msanii huyu mpaka leo hana mtoto, may b inawezekana kuwa hiyo ikawa ni sabbu.

2.Queen Latipha
Msanii mwingine ni Female Hip Pop Artist, Queen Latipha mwenye miaka 42. yeye anasema kuwa alibakwa na kijana ambaye alikuwa akimuangalia, kibongo bongo tunaweza kusema house boy.
Hivi karibuni Queen Latipha alisema kuwa ana mpango wa kuadopt mtoto huku Afrika.

 3.Oprah Winfrey
Katika list ya mastaa wa kike waliowahi kubakwa utotoni mwingine ni mtangazaji maarufu duniani na muigizaji pia, Oprah Winfrey mwenye takribani miaka kama 58 hivi yeye alibakwa kama mara 3 hivi.
 Oprah.
Mara ya kwanza alibakwa akiwa na miaka 9 na binamu/cousin wake mwenye umri wa miaka 19, cousin huyo aliachwa ili amwangalie Oprah, baada ya kumbaka akaenda kumnunulia Ice cream nakumwambia akae kimya asimwambie mtu, na akakubali.Baadae akaja kubakwa tena na rafiki wa familia na uncle wake, na yote akapiga kimya.Akiwa na miaka 13 baada ya kuchoka manyanyaso hayo Oprah akatoroka nyumbani, na akapata ujauzito akiwa na miaka 14 ambapo mtoto wake alikufa tu baada ya kuzaliwa.

Vyote hivyo alisema kuwa ndo sababu ambayo imemfanya mpaka leo asiwe na mtoto na amesema kuwa ameamua kutokuwa mama kwasababu yeye hakulelewa vizuri.

 4.Missy Elliot
Rappa mwingine wa kike ambaye alifanya vizuri katika gemu Missy Elliot ni kati ya mastaa ambao waliwahi kubakwa.Missy alibakwa akiwa na mika 8 na cousin wake mwenye umri wa miaka 16, kila baada ya Missy kutoka shule binamu yake huyo alikuwa akimfanyia vitendo hivyo, na vitendo hivyo viliendelea bila kwa muda bila ya yeye kumwambia mtu.
  Missy Elliot.
Missy Eliot aliwahi kusema kuwa hana mpango wa kupata mtoto siku za hivi karibuni kwasabbu anaogopa uchungu wa labour.

5.Fantansia Barrino.
Katika list hii pia yupo mwanadada ambaye alikuwa ni mshindi wa American Idol mwaka 2004 , Fantansia Barrino.Akiwa high School na miaka 14 Msanii huyu mwenye umri wa miaka 28 hivi sasa, alibakwa shuleni, kitu amabcho kilimfanya ajisikie vibaya, coz alichekwa na wenzake na wanaume wengine wakamwambia kuwa na wao iko siku watafanya hivyo kitendo ambacho kilimfanya Fantansa aache shule.
Fantansia na mtoto wake wa kike. 
Fantansi aliingia mtaani na akiwa na miaka 17 akapata ujauzito, nakupata mtoto wake wa kike.

No comments: