Selenga Kaduma
Hawa ndo Artist wenye VVU Doll South kwa sasa.
Mad P Upete
Obby Maphiyonso
Brana Radium
Timmy San
Dogo Scope
Mgc Mtata
Smacka Mtata
Meda
Echa Da Charlie
Ney Lee
Wisma
Jay Mutta
Man Kichef
Med C
&
Man King
NB: VVU manaa ake VINA VIKALI USIPIME.
Dogo Janja
Serikali
hakuna kuanzia leo siwapendi Traffic na sababu ninazo mimi naenda shule
nipo kwny Daladala alaf eti dereva wa gari yetu kazuia Njia eti na
abiria tumepelekwa police nauli zetu haturudishiwi mi nimekaza nipo
kituoni Ubungo hapa tumegoma wamesema wanatupeleka mpk mwenge alaf
Trafic anaongea lugha chafuu imenipain sana dah! Siwapendi trafic
wamenichelewesha shule wametupiga mikwara siwapendiii tena narudia
-
Ruwaa'ichi Minja
MATESO YA VENGU, WACHAWI NI ORIJINO KOMEDI WENYEWE
MUIGIZAJI Joseph Shamba ‘Vengu’, (wa kwanza kulia) ameugua kwa muda
mrefu. Ukitazama tukio la msanii huyo kuumwa, unaweza kuhisi kuwa
wenzake kwenye kundi hilo walikuwa pamoja naye. Si kweli, wao ndiyo
sababu ya mateso yake. Vengu hajawahi kuwa na furaha akiwa na Kundi la
Orijino Komedi. Wenzake walimtenga na kumfanyia mambo mengi ya kuumiza.
Maskini ya Mungu, Vengu akaona kujipoza na machungu ya kutengwa,
kunyanyaswa na wenzake ni kuwa mlevi. Makala haya, shabaha yake ni
kuwafanya Orijino Komedi kuwa wamoja. Wajione kwamba kila mmoja kwenye
kundi hilo ana haki sawa. Si kubaguana na kutendeana mambo ya kuumiza
kama alivyotendwa Vengu kwa muda mrefu. Kama memba wengine wa Orijino
Komedi, Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’, Mjuni Silvery ‘Mpoki’, Lucas
Mhuvile ‘Joti’, Emanuel Mgaya ‘Masanja’ na Alex Chalamila ‘McRegan’
wangemfanya Vengu kuwa sehemu ya maisha yao, asingeteseka kama
ilivyotokea.
Ingewezekana kabisa kwa memba wa kundi hilo kumpa
faraja, badala ya kumtenga na kumsababishia aishi kwa mawazo. Kitendo
cha kumbagua kilisababisha aone pombe ndiyo kimbilio lake. Kabla
hajazidiwa, alipenda kulewa akiamini ndiyo faraja yake. Mimi na Vengu
tumewahi kufanya vikao kadhaa na kuzungumzia yale yanayomsibu. Alipenda
sana kuficha ukweli unaomuumiza kwamba kuna baadhi ya wasanii wenzake
wanamtenda ndivyo sivyo. Maskini Vengu, namuombea kwa Mungu azidi kumpa
afua, apone kabisa. Mungu mwingi wa rehema zote, kubwa na ndogo,
atamponya Vengu. Bila shaka atarudi kwenye hali yake ya kawaida.
Ninaamini kuwa hata hali yake ya kutawaliwa na msongo wa mawazo,
itapona. Hatakuwa mlevi tena kama ilivyokuwa mwanzo. Ugonjwa wa Vengu
una matawi mengi. Kwa nafasi yangu ya uandishi wa habari pendwa,
nilinasa taarifa za awali kuhusu kuumwa kwa Vengu. Kuna baadhi ya watu
hawakutaka kuelewa chochote zaidi ya kushikilia kwamba msanii huyo
ameshughulikiwa na wenzake. Yupo msanii mmoja wa Kundi la Orijino Komedi
alitajwa mno. Hata hivyo, hilo la uchawi sikulipa nafasi ndiyo maana
hata habari hiyo hatukuwahi kuiripoti. Sisi Global Publishers
tumestaarabika, hatuamini uchawi. Nilimshauri mtoa habari akazanie
huduma za hospitali.
Wakati huo Vengu amelazwa Hospitali ya
Taifa, Muhimbili. Mara kadhaa nyakati za jioni, nilikutana na mtoa
habari za uchawi (kwamba msanii wa kundi hilo kamroga Vengu). Kwa
busara, nikawa namshauri taratibu ili aondokane na imani hizo. Nauchukia
ushirikina. Hata hivyo, wakati mwingine inakuwa rahisi kupata picha
kuwa mtindo wa maisha ya wasanii hao dhidi ya mwenzao ndiyo sababu ya
kuibuka kwa hisia za uchawi. Wangempenda na kumjali siku zote ndani ya
kundi hilo, asingehisi kama anarogwa. Ndugu na rafiki zake,
wasingewahisi vibaya wenzake. Sijawahi kusikia malalamiko kutoka kwa
ndugu zake wakisema Vengu amerogwa. Zaidi marafiki ndiyo walikuwa
wakieneza habari hizo. Inawezekana kwa marafiki kwa sababu ndiyo
aliochangia nao mazungumzo na hata vikao vya baa. Bila shaka, hata wale
marafiki zake waliokuwa hawataki kuelewa kwamba Vengu anaumwa na siyo
uchawi, leo hii watakuwa mashahidi. Kwa wakati ule, kuna mtu (simtaji
jina kwa sasa), alinishutuma kwamba mimi ni muoga, eti kwa sababu
nilisema sitaandika habari ya Vengu kurogwa. Awamu nyingine niliambiwa
nimehongwa.
Tuhuma zote hizo nilizibeba kwa sababu sikutaka
niwaridhishe watu kwa muda, nikasahu maumivu ya baadaye itakapothibitika
kwamba niliandika habari ya uongo ambayo sitaweza kuitetea. Siku zote
uchawi hauthibitishiki. Wakati mwingine nilicheka kwa sababu sikumuona
mwenye ubavu wa kunihonga kuzuia habari hiyo. Nilikataa habari kwa maana
ingeweza kuibua matokeo mabaya. Kusema Vengu amerogwa kwa hali
aliyokuwa nayo, ni uchochezi usiovumilika. Unaweza kumuona Vengu ni wa
kawaida kwako, lakini kwa wengine (hususan wazazi na ndugu zake) ni kila
kitu kwao. Kuandika Vengu amerogwa, siyo tu ingeibua chuki kati ya
ndugu zake na wasanii wa Orijino Komedi, bali pia ndugu wangeweza
kumtorosha kumpeleka kwa ‘babu’. Sisi Global huwa tunaangalia maeneo
yote hayo kabla ya kuchapisha habari zetu. Hekima hizo ndizo
zimetufikisha hapa tulipo. Kila habari inapimwa kwenye mzani, pumba
zinawekwa pembeni halafu ukweli unatangulizwa mbele. Leo ninapogusia
uchawi, namaanisha kwamba wasanii wa kundi hilo wanatakiwa kuishi
vizuri. Wasitengane, kwani hali hiyo ndiyo chanzo cha kuibua hisia mbaya
miongoni mwao. Orijino Komedi wanapaswa kujirudi kwa Vengu.
Je, unajua kwamba wakati wasanii wa kundi hilo wakiwa bado wanafanya
kazi zao kwenye Televisheni ya Channe 5 (EATV), walipewa nyumba ya
kuishi na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi? Nyumba hiyo
ipo Kunduchi, Dar es Salaam. Vengu alifukuzwa kwenye nyumba hiyo,
akiwaacha wenzake wanatanua. Habari hiyo iliandikwa, kumbukumbu tunazo.
Haikuishi hapo, walipohamia TBC1, walipewa magari lakini baada ya muda
mfupi, Vengu alinyng’anywa gari, akawa anatembea kwa daladala, wenzake
wana magari yao. Utakubaliana na mimi kwamba wasanii wenzake walimpa
unyonge mkubwa kiasi kwamba mwenyewe akawa hana la kutuliza akili zaidi
ya kunywa pombe. Tuna mlolongo wa matukio mengi ya msanii huyo
kuharibikiwa baada ya kuzidiwa na kiwango kikubwa cha pombe
alichokunywa. Ametendwa sana!.............posted by deejay jona

Selenga Kaduma
Hawa ndo Artist wenye VVU Doll South kwa sasa.
Mad P Upete
Obby Maphiyonso
Brana Radium
Timmy San
Dogo Scope
Mgc Mtata
Smacka Mtata
Meda
Echa Da Charlie
Ney Lee
Wisma
Jay Mutta
Man Kichef
Med C
&
Man King
NB: VVU manaa ake VINA VIKALI USIPIME.
Mad P Upete
Obby Maphiyonso
Brana Radium
Timmy San
Dogo Scope
Mgc Mtata
Smacka Mtata
Meda
Echa Da Charlie
Ney Lee
Wisma
Jay Mutta
Man Kichef
Med C
&
Man King
NB: VVU manaa ake VINA VIKALI USIPIME.

Dogo Janja
Serikali
hakuna kuanzia leo siwapendi Traffic na sababu ninazo mimi naenda shule
nipo kwny Daladala alaf eti dereva wa gari yetu kazuia Njia eti na
abiria tumepelekwa police nauli zetu haturudishiwi mi nimekaza nipo
kituoni Ubungo hapa tumegoma wamesema wanatupeleka mpk mwenge alaf
Trafic anaongea lugha chafuu imenipain sana dah! Siwapendi trafic
wamenichelewesha shule wametupiga mikwara siwapendiii tena narudia

- Ruwaa'ichi MinjaMATESO YA VENGU, WACHAWI NI ORIJINO KOMEDI WENYEWE
MUIGIZAJI Joseph Shamba ‘Vengu’, (wa kwanza kulia) ameugua kwa muda mrefu. Ukitazama tukio la msanii huyo kuumwa, unaweza kuhisi kuwa wenzake kwenye kundi hilo walikuwa pamoja naye. Si kweli, wao ndiyo sababu ya mateso yake. Vengu hajawahi kuwa na furaha akiwa na Kundi la Orijino Komedi. Wenzake walimtenga na kumfanyia mambo mengi ya kuumiza. Maskini ya Mungu, Vengu akaona kujipoza na machungu ya kutengwa, kunyanyaswa na wenzake ni kuwa mlevi. Makala haya, shabaha yake ni kuwafanya Orijino Komedi kuwa wamoja. Wajione kwamba kila mmoja kwenye kundi hilo ana haki sawa. Si kubaguana na kutendeana mambo ya kuumiza kama alivyotendwa Vengu kwa muda mrefu. Kama memba wengine wa Orijino Komedi, Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’, Mjuni Silvery ‘Mpoki’, Lucas Mhuvile ‘Joti’, Emanuel Mgaya ‘Masanja’ na Alex Chalamila ‘McRegan’ wangemfanya Vengu kuwa sehemu ya maisha yao, asingeteseka kama ilivyotokea.
Ingewezekana kabisa kwa memba wa kundi hilo kumpa faraja, badala ya kumtenga na kumsababishia aishi kwa mawazo. Kitendo cha kumbagua kilisababisha aone pombe ndiyo kimbilio lake. Kabla hajazidiwa, alipenda kulewa akiamini ndiyo faraja yake. Mimi na Vengu tumewahi kufanya vikao kadhaa na kuzungumzia yale yanayomsibu. Alipenda sana kuficha ukweli unaomuumiza kwamba kuna baadhi ya wasanii wenzake wanamtenda ndivyo sivyo. Maskini Vengu, namuombea kwa Mungu azidi kumpa afua, apone kabisa. Mungu mwingi wa rehema zote, kubwa na ndogo, atamponya Vengu. Bila shaka atarudi kwenye hali yake ya kawaida. Ninaamini kuwa hata hali yake ya kutawaliwa na msongo wa mawazo, itapona. Hatakuwa mlevi tena kama ilivyokuwa mwanzo. Ugonjwa wa Vengu una matawi mengi. Kwa nafasi yangu ya uandishi wa habari pendwa, nilinasa taarifa za awali kuhusu kuumwa kwa Vengu. Kuna baadhi ya watu hawakutaka kuelewa chochote zaidi ya kushikilia kwamba msanii huyo ameshughulikiwa na wenzake. Yupo msanii mmoja wa Kundi la Orijino Komedi alitajwa mno. Hata hivyo, hilo la uchawi sikulipa nafasi ndiyo maana hata habari hiyo hatukuwahi kuiripoti. Sisi Global Publishers tumestaarabika, hatuamini uchawi. Nilimshauri mtoa habari akazanie huduma za hospitali.
Wakati huo Vengu amelazwa Hospitali ya Taifa, Muhimbili. Mara kadhaa nyakati za jioni, nilikutana na mtoa habari za uchawi (kwamba msanii wa kundi hilo kamroga Vengu). Kwa busara, nikawa namshauri taratibu ili aondokane na imani hizo. Nauchukia ushirikina. Hata hivyo, wakati mwingine inakuwa rahisi kupata picha kuwa mtindo wa maisha ya wasanii hao dhidi ya mwenzao ndiyo sababu ya kuibuka kwa hisia za uchawi. Wangempenda na kumjali siku zote ndani ya kundi hilo, asingehisi kama anarogwa. Ndugu na rafiki zake, wasingewahisi vibaya wenzake. Sijawahi kusikia malalamiko kutoka kwa ndugu zake wakisema Vengu amerogwa. Zaidi marafiki ndiyo walikuwa wakieneza habari hizo. Inawezekana kwa marafiki kwa sababu ndiyo aliochangia nao mazungumzo na hata vikao vya baa. Bila shaka, hata wale marafiki zake waliokuwa hawataki kuelewa kwamba Vengu anaumwa na siyo uchawi, leo hii watakuwa mashahidi. Kwa wakati ule, kuna mtu (simtaji jina kwa sasa), alinishutuma kwamba mimi ni muoga, eti kwa sababu nilisema sitaandika habari ya Vengu kurogwa. Awamu nyingine niliambiwa nimehongwa.
Tuhuma zote hizo nilizibeba kwa sababu sikutaka niwaridhishe watu kwa muda, nikasahu maumivu ya baadaye itakapothibitika kwamba niliandika habari ya uongo ambayo sitaweza kuitetea. Siku zote uchawi hauthibitishiki. Wakati mwingine nilicheka kwa sababu sikumuona mwenye ubavu wa kunihonga kuzuia habari hiyo. Nilikataa habari kwa maana ingeweza kuibua matokeo mabaya. Kusema Vengu amerogwa kwa hali aliyokuwa nayo, ni uchochezi usiovumilika. Unaweza kumuona Vengu ni wa kawaida kwako, lakini kwa wengine (hususan wazazi na ndugu zake) ni kila kitu kwao. Kuandika Vengu amerogwa, siyo tu ingeibua chuki kati ya ndugu zake na wasanii wa Orijino Komedi, bali pia ndugu wangeweza kumtorosha kumpeleka kwa ‘babu’. Sisi Global huwa tunaangalia maeneo yote hayo kabla ya kuchapisha habari zetu. Hekima hizo ndizo zimetufikisha hapa tulipo. Kila habari inapimwa kwenye mzani, pumba zinawekwa pembeni halafu ukweli unatangulizwa mbele. Leo ninapogusia uchawi, namaanisha kwamba wasanii wa kundi hilo wanatakiwa kuishi vizuri. Wasitengane, kwani hali hiyo ndiyo chanzo cha kuibua hisia mbaya miongoni mwao. Orijino Komedi wanapaswa kujirudi kwa Vengu.
Je, unajua kwamba wakati wasanii wa kundi hilo wakiwa bado wanafanya kazi zao kwenye Televisheni ya Channe 5 (EATV), walipewa nyumba ya kuishi na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi? Nyumba hiyo ipo Kunduchi, Dar es Salaam. Vengu alifukuzwa kwenye nyumba hiyo, akiwaacha wenzake wanatanua. Habari hiyo iliandikwa, kumbukumbu tunazo. Haikuishi hapo, walipohamia TBC1, walipewa magari lakini baada ya muda mfupi, Vengu alinyng’anywa gari, akawa anatembea kwa daladala, wenzake wana magari yao. Utakubaliana na mimi kwamba wasanii wenzake walimpa unyonge mkubwa kiasi kwamba mwenyewe akawa hana la kutuliza akili zaidi ya kunywa pombe. Tuna mlolongo wa matukio mengi ya msanii huyo kuharibikiwa baada ya kuzidiwa na kiwango kikubwa cha pombe alichokunywa. Ametendwa sana!.............posted by deejay jona
No comments:
Post a Comment