‘WEUSI’ jina ambalo limefunika sana kwenye playlist za media
mbalimbali kwa mwaka huu, sasa wameamua kuufunga mwaka kwa aina ya pekee,
ambapo wanatarajiwa kupiga show kali ya kuufunga ukurasa wa mwaka huu Jumapili
hii(December, 23) pale Maisha Club.
Lord eyez atawasapraiz fans wake kama alivyowaahidi kwenye
press conference aliyoiitisha hivi karibuni baada ya matatizo aliyopata, ambapo
ngoma yake mpya ya
‘Mapito’ inayosubiriwa kwa hamu itasikika usiku huo.
Kitu kingine kikubwa ni uzinduzi wa DVD ya Nikki wa Pili
‘Kum Kubam’ jina ambalo limesumbua pia kwenye zile ngoma zenye element zote za
Hip Hop.
Mweusi G-Nako ameiambia Leotainmenttz.com kuwa sababu za kuliita ‘Funga Mwaka la Weusi’
ni matukio makubwa yatakayofanyika usiku huo, uzinduzi wa wimbo wa Lord Eyez
ambao unasubiriwa kwa hamu, Uzinduzi wa DVD ya Kum Kubam, na kwa mara ya kwanza
watu watashuhudia aina mpya ya usambazaji wa kazi za wasanii. Hii ni aina gani
tena? Tutaifahamu tu jumapili.
G-Warawara amewaahidi fans wao kuwa watashuhudia ‘show ya
milele’ toka kwa safu ya WEUSI, JOH MAKINI, NIKKI WA PILI, BONTA, LORD EYEZ NA
YEYE MWENYEWE G-NAKO.
Kiingilio katika show hiyo itakuwa sh. 10,000/- TU
No comments:
Post a Comment