Sunday, January 20, 2013

Msanii Nyota Ndogo atuhumiwa kuiba wimbo wa msanii mchanga, inasemekana aliiusikiliza studio


Kwa hapa bongo imekuwa kama ni story za kawaida sasa hasa kwa wasanii wachanga kuwalalamikia wasanii wakubwa kuiba idea zao ama nyimbo zao na kufanya hits. Huko Kenya pia imemtokea msanii wa kike aliyehustle kutoka kuwa mfanyakazi wa ndani hadi kuwa staa.

Nyota Ndogo anatuhumiwa na msanii chipukizi wa Nchini Kenya rapper toka mitaa ya Nairobi anaeitwa Kachela Kroma, na wimbo ambao unaleta haya yote unaitwa 'Tunataka Amani'.

Kachela alifunguka kuwa aliandika wimbo huo baada ya machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007, na akaurekodi wimbo huo na msanii mwenzake anaeitwa Bunsen B katika studio iliyoko Nairobi ambayo kwa sasa inaitwa Ketebul Music enzi hizo ilikuwa inaitwa Ketebu Production na producer mtanzania mwenyeji wa Mwanza Jesse Bukindu ambae hivi sasa ni rafiki wa karibu wa Nyota ndogo.
Rapper huyo chipukizi amemrushia mpira wa lawama producer Jesse kuwa alikuwa na tabia ya kuucheza wimbo huo mara kwa mara na kuwasikilizisha watu mbalimbali waliofika pale studio akiwemo Nyota Ndogo na hapo ndipo anaamini Nyota ndogo aliukwapua na kuuweka kichwani.

No comments: