Wednesday, March 6, 2013

EXCLUSIVE KUTOKA KWA VICENT KIGOSI AKA RAY


Picha hiyo ya kushoto inamuonesha Ray wa mwanzo na  kulia ikionyesha Ray wa sasa
Muigizaji ambae anafanya poa sana katika soko la filamu hapa Bongo na aliyepo kwenye list A ya waigizaji wa filamu Tanzania, muite Vincent Kigosi maarufu kwa jina la Ray , ameamua kuzungumza baada ya watu kuanza kumzushia anaumwa kutokana na kupungua mwili wake kwa kiasi kikubwa.

Ray amezikanusha tetesi hizo zilizoanza kusambaa kwa haraka ambapo gazeti la udaku la Kiu wiki hii lilikuwa na habari isemayo, ‘Ray apukutika mwili’ – Kitambi chote kwishnei! Ukimuona unaweza kumpita bila kumtambua, maombi ya wakatoliki yahusishwa.

Hata hivyo Ray amesema hali hiyo imetokana na kufanya mazoezi zaidi siku za hivi karibuni. “Jamani kwani unene ndio afya au kupungua ndio ugonjwa,” ameuliza Ray.

No comments: