EXLUSIVE YA KALA JEREMIAH
KALA JEREMIAH
MWAKA
2011 MIMI KWA KUSHIRIKIANA NA ROMA TULIANZISHA TOUR YENYE LENGO LA
KUWAFIKIA WATANZANIA KOTE NCHINI HASA WAKULIMA, WAFUGAJI, WAVUVI,
WACHIMBAJI WADOGOWADOGO WA MADINI,NA WATU WENGINE WA AINA HIYO. LENGO LA
SISI KUFANYA HIVYO ILIKUWA NI SISI KUONGEA NA WATU KUJUA CHANGAMOTO
WANAZOKUTANA NAZO KATIKA MAISHA YA KILA SIKU,PIA KUJUA UMASKINI HALISI
WA MTANZANIA.KUJUA HISIA ZAO, MAONI YAO, NA NINI WANGEPENDA KIFANYIKE,.
PROJECT HII ILIKUWA NA MAMBO MENGI SANA.TULIFANIKIWA KUANZA NA KANDA YA
ZIWA AMBAKO TULIFANIKIWA KUKUTANA NA WAVUVI, WACHIMBAJI WADOGOWADOGO WA
MADINI,NA WATU WAISHIO KARIBU NA MIGODI. KWA KUWA ILIKUWA NI MWANZO
TULIISHIA HAPO KWANZA NA TULISITISHA KUTOKANA NA KUBANWA NA MAJUKUMU
MENGINE YA KIKAZI LAKINI IKIWA NI PAMOJA NA UFINYU WA BAJETI KWA KUWA
TULIKUWA TUNATUMIA HELA ZETU NA HATUKUWA NA MDHAMINI.
PROJECT HII IKO HAI NA ITAENDELEA TENA MWAKA HUU KWA KISHINDO.
LAKINI WAKATI TUNAFANYA PROJECT HII NILIGUNDUA PIA KUWA VIJANA WENGI
WAISHIO MAENEO TULIYOYATEMBELEA WANAAMINI KUWA ILI WAFANIKIWE NI LAZIMA
WAJE DAR YANI WANAAMINI DAR ES SALAM NDO SEHEMU YA KUTOKEA KI MAISHA,
HILO MIMI BINAFSI SIKULIPENDA HATA KIDOGO NA KWA KUWA MIMI NAISHI DAR NA
NAJUA KUWA DAR KUNA WATU WANAMAISHA MAGUMU SANA. KWA HIYO NILIPORUDI
DAR NILIFANYA UCHUNGUZI USIO RASMI WA MAISHA HALISI YA MTU WA KAWAIDA
WA DAR NILIYOYAGUNDUA KWENYE UCHUNGUZI HUO NILIYAANDIKA YOOTE NA
KUYATENGENEZEA WIMBO UNAOITWA KARIBU DAR.
KARIBU DAR
NIMEJITAHIDI KUONGEA UKWELI WA MAISHA HALISI YA WATU WA KAWAIDA WA DAR.
LENGO LA KUFANYA WIMBO HUU NI KUTAKA KUMJULISHA MTU ALIYEKO SEHEMU
NYINGINE NA ANAAMINI KUWA DAR NDO SEHEMU PEKEE ATAKAYOTOKEA KI
MAISHA.KWA KIFUPI KARIBU DAR NI WIMBO UNAOELEZEA MAISHA MAGUMU YA WATU
WA KAWAIDA WA DAR LENGO LA KUFANYA WIMBO HUU NI KUHAMASISHA VIJANA WAKAE
WALIPO NA WAZITUMIE VIZURI FURSA WALIZONAZO KULIKO KUKAA NA KUOTA KUWA
DAR NDO KUNA MAISHA MAZURI.
WIMBO HUU NIMESHIRIKIANA NA MKALI
WA RNB BEN POL NA WIMBO UKO TAYARI NA UMEFANYIKA KWENYE STUDIO ZA SMART
MUSSIC CHINI YA MUANDAAJI PRODUCER MBEZI NA VIDEO YAKE IMEFANYIKA NEXT
LEVEL CHINI YA DIRECTOR ADAM JUMA KILA KITU KIKO SAWA SO KAA MKAO WA
KULA KUANZIA WIKI IJAYO KINANUKA.NAOMBA MAPOKEZI YAKO. ASANTE SANA
No comments:
Post a Comment