Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiwa na msafara wake
wakikagua ujenzi unaoendelea wa daharia (bweni) katika shule ya
sekondari Kasanga. Mradi huo ni sehemu ya miradi inayofadhiliwa na mradi
wa usimazi wa ziwa Tanganyika uliopo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais
Mazingira pamoja na miradi mingine ya ya ujenzi wa vyumba vitatu vya
madarasa katika shule ya msingi Muzi na ujenzi wa wadi ya kujifungulia
kinamama kijiji cha Samazi. Miradi yote hiyo itawanufaisha wakazi wa
mwambao wa ziwa Tanganyika na inagharimu zaidi ya shilingi milioni 150.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Samazi mwambao
na ziwa Tanganika alipofika kukagua ujenzi wa wadi ya kujifungulia
kinamama katika kijiji hicho. Mkuu huyo wa Mkoa alimuagiza Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kuwafuatilia kwa karibu wahandisi
wanaojenga miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati. Aliwaasa pia
wananchi kuzingatia uzazi wa mpango katika kuboresha maisha yao pamoja
na kuwaendelezea watoto wao kielimu tofauti na hali ilivyo hivi sasa
ambapo muamko wa elimu Mkoani Rukwa upo chini. Aliwataka pia kuboresha
hali ya ulinzi katika maeneo yao ya mipakani kwa kutokuwakaribisha
wageni bila kuwa na taarifa zao za kutosha.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa na msafara wake wakikagua ujenzi wa madarasa matatu
katika shule ya Msingi Muzi yaliyowekwa jiwe la msingi na Naibu Waziri
wa TAMISEMI Aggrey Mwanri ambayo mpaka kukamilika kwake yatagharimu
zaidi ya shilingi Milioni 50.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na wanafunzi wa
shule ya msingi Muzi iliyopo pembezoni mwa Ziwa Tanganyika Mkoani Rukwa
baada ya kukagua ujenzi unaoendelea wa madara yanayofadhiliwa na mradi
wa usimamizi wa ziwa Tanganyika mradi ambao upo chini ya Ofisi ya Makamu
wa Rais Mazingira. Aliwaasa wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuwaahidi
kuwapa ushirikiano wale watakaofaulu vizuri na kukosa uwezo wa
kujiendeleza.
Sehemu
ya fukwe ya Ziwa Tanganyika katika kijiji cha Samazi Mkoani Rukwa
ambapo mradi wa usimamizi wa ziwa Tanganyika unatekeleza mradi wa ujenzi
wa wadi ya kinamama kwa ajili ya kujifungulia katika Zahanati ya kijiji
hicho.
(NA HAMZA TEMBA – OFISI YA MKUU WA MKOA RUKWA
No comments:
Post a Comment